2 Baba mkwe wake akamwambia, “Nilikuwa na hakika kwamba ulimchukia, hivyo nikampeana kwa rafiki yako. Je, dada yake mdogo si mzuri kuliko yeye? Mchukue huyo badala yake.”
3 Samsoni akawaambia, “Wakati huu, nitakapowadhuru Wafilisti, sitakuwa na lawama.” 4 Hivyo Samsoni akaondoka na kuwakamata mbweha mia tatu, akawafunga wawili wawili, mikia kwa mikia. Kisha akafungia mwenge wa moto kwenye kila jozi la mikia hiyo. 5 Akawasha ile mienge na kuwaachia wale mbweha katika mashamba ya Wafilisti ya nafaka zilizosimamishwa katika matita. Akateketeza matita ya nafaka, pamoja na mashamba ya mizabibu na mashamba ya mizeituni.
6 Wafilisti walipouliza, “Ni nani aliyetenda jambo hili?” Wakaambiwa, “Ni Samsoni, mkwewe yule Mtimna, kwa sababu mkewe alipeanwa kwa rafiki yake.”
9 Wafilisti wakapanda na kupiga kambi huko Yuda na kuenea huko Lehi. 10 Watu wa Yuda wakawauliza, “Kwa nini mmekuja kupigana nasi?”
11 Ndipo watu elfu tatu wa Yuda waliteremka hadi kwenye pango katika mwamba wa Etamu, wakamwambia Samsoni, “Je, hujatambua kuwa Wafilisti wanatutawala? Ni nini hiki ulichotutendea?”
12 Wakamwambia, “Tumekuja kukufunga na kukutia mikononi mwa Wafilisti.”
13 Wakamjibu, “Sisi hatutakuua, bali tutakufunga tu na kukutia mikononi mwao.” Basi wakamfunga kwa kamba mbili mpya na kumchukua toka huko kwenye pango katika mwamba. 14 Alipokaribia Lehi, Wafilisti wakamjia wakipiga kelele. Roho wa Mwenyezi Mungu akaja juu yake kwa nguvu. Kamba zilizomfunga mikono zikawa kama kitani iliyochomwa kwa moto, na vifungo vyake vikaanguka chini toka mikononi mwake. 15 Ndipo akaona mfupa mpya wa taya la punda, akanyoosha mkono, akauchukua na kuua nao Wafilisti wapatao elfu moja.
16 Ndipo Samsoni akasema,
18 Kwa kuwa alihisi kiu sana, akamlilia Mwenyezi Mungu, akisema, “Umempa mtumishi wako ushindi huu mkuu. Je, sasa nife kwa kiu na kuangukia mikononi mwa hawa watu wasiotahiriwa?” 19 Ndipo Mungu akafunua shimo huko Lehi, na maji yakatoka. Samsoni alipoyanywa maji hayo, nguvu zikamrudia, akahuika. Hivyo chemchemi ile ikaitwa En-Hakore[b], nayo iko hadi leo huko Lehi.
20 Samsoni akawa mwamuzi wa Waisraeli katika siku za Wafilisti kwa muda wa miaka ishirini.
<- Waamuzi 14Waamuzi 16 ->
Languages