3 Baba yake na mama yake wakamjibu, “Je, hakuna mwanamke miongoni mwa jamaa yako au miongoni mwa watu wetu wote, hata ulazimike kwenda kujitwalia mke kutoka kwa hao Wafilisti wasiotahiriwa?”
8 Baada ya muda, Samsoni aliporudi ili akamwoe, akageuka kando ili kuutazama mzoga wa yule simba. Tazama! Ndani ya ule mzoga akaona kundi la nyuki na asali kiasi. 9 Akachukua asali mkononi mwake, akala huku akitembea. Alipowafikia baba yake na mama yake, akawapa kiasi cha ile asali, nao wakala. Lakini hakuwaambia kuwa aliitwaa asali katika mzoga wa simba.
10 Basi baba yake akateremka kumwona huyo mwanamke. Samsoni akafanya karamu huko, kama ilivyokuwa desturi ya vijana. 11 Watu walipomwona, wakaleta vijana wenzake thelathini ili kuwa pamoja naye.
12 Samsoni akawaambia, “Niwape kitendawili, mkiweza kunipa jibu katika muda wa siku hizi saba za karamu, nitawapa mavazi thelathini ya kitani na mavazi mengine mivao thelathini. 13 Lakini msipoweza kufumbua, ndipo ninyi mtanipa mavazi thelathini ya kitani na mavazi mengine mivao thelathini.”
14 Akawaambia,
15 Siku ya nne, wakamwambia mkewe Samsoni, “Mbembeleze mumeo ili atutegulie hicho kitendawili, la sivyo tutakuchoma moto wewe na wa nyumba ya baba yako. Je, mmetualika ili mpate kutunyang’anya kile tulicho nacho?”
16 Basi mke wa Samsoni akalia mbele yake na kumwambia, “Unanichukia! Hunipendi kabisa. Umewategea watu wangu kitendawili, lakini mimi hujaniambia jibu.”
18 Siku ya saba, kabla ya jua kutua, wanaume wa mji wakamwambia Samsoni,
19 Ndipo Roho wa Mwenyezi Mungu akamjia Samsoni kwa nguvu. Samsoni akateremka hadi Ashkeloni, akawaua wanaume thelathini wa mji huo, akatwaa mali yao, akawapa watu wale waliotegua kile kitendawili nguo zao. Akiwa amejaa hasira, akakwea kurudi nyumbani kwa baba yake. 20 Naye mke wa Samsoni akakabidhiwa kwa rafiki yake Samsoni aliyekuwa msaidizi wake siku ya arusi.
<- Waamuzi 13Waamuzi 15 ->
Languages