Link to home pageLanguagesLink to all Bible versions on this site
70
Kwa kiongozi wa muziki. Zaburi ya Daudi; kuleta kumbukumbu. 1 Uniokoe, Mungu! Yahwe, njoo haraka na unisaidie mimi. 2 Wale wajaribuo kuchukua uhai wangu waaibishwe na kufedheheshwa; warudishwe nyuma na wasiheshimiwe, wale wafurahiao katika maumivu yangu. 3 Warudishwe nyuma kwa sababu ya aibu yao, wale wasemao, “Aha, aha.” 4 Wale wakutafutao wafurahi na kushangilia katika wewe; wale waupendao wokovu wako siku zote waseme, “Mungu asifiwe.” 5 Lakini mimi ni maskini na muhitaji; harakisha kwangu, Mungu; wewe ni msaada wangu nawe huniokoa mimi. Yahwe, usichelewe.

<- Zaburi 69Zaburi 71 ->
  • Zaburi