7
Utungo wa muziki wa daudi, ambao alimwimbia Yahwe kuhusu maneno ya Cush Mbenjamini 1 Yahweh Mungu wangu, kwako napata kimbilio! Uninusuru na hao wote wanikimbizao, na uniokoe. 2 Vinginevyo, watanipura kama simba, na kunitawanya viapande vipande na asiwepo mtu wa kuweza kunirudisha katika usalama. 3 Yawheh Mungu wangu, Sijawahi kufanya kile maadui zangu wanacho sema nilifanya; sina hatia katika mikono yangu. 4 Sijawahi kumkosea mtu yeyote aliye na amani na mimi, au kumdhuru kipumbavu yeyote aliye kinyume na mimi. 5 Ikiwa sisemi ukweli basi umruhusu adui yangu kuyaingilia maisha yangu na kuyaharibu; na umuache aukanyage mwili wangu ulio hai kwenye aridhi na kuuacha umelala kwa aibu mavumbini. Selah 6 Inuka, Yahweh, katika hasira yako; simama kinyume na hasira kali ya adui zangu; amka kwa ajili yangu na ubebe amri zako ambazo wewe umeamuru kwa ajili yao. 7 Mataifa yote yamekuzunguka; uwatawale kutoka mbinguni. 8 Yahweh, uwahukumu mataifa; uwaonyeshe kuwa sina hatia, Yahweh, kwa sababu mimi ni mwenye haki na sina hatia, Ewe uliye juu. 9 Matendo ya waovu na yafike mwisho, bali uanzishe watu wenye haki, Mungu mwenye haki, wewe ambaye unapima mioyo na fahamu. 10 Ngao yangu inatoka kwa Mungu, yule anaye okoa moyo wa mwenye haki. 11 Mungu ni mwamuzi mwenye haki, Mungu anaye chukizwa na waovu kila siku. 12 Ikiwa kuna mtu hatubu, Mungu atanoa upanga wake na ata andaa upinde wake kwa ajili ya vita. 13 Ana jiandaa kutumia siraha kupambana naye; anatengeneza mishale yake kuwa ya moto. 14 Fikiria kuhusu huyo ambaye ana ujauzito wa maovu, mwenye mimba ya mipango ya uharibifu, anaye zaa sumu ya uharibifu. 15 Yeye huchimba shimo na kuliacha wazi kisha baadaye hudumbukia katika shimo alilochimba mwenyewe. 16 Mipango yake mwenyewe ya uharibifu hugeukia kichwa chake mwenyewe, kwa kuwa vurugu zake mwenyewe humshukia kichwani pake. 17 Kwa haki yako Mungu nitakushukuru; nitaimba sifa kwa Mungu aliye juu.
<- Zaburi 6Zaburi 8 ->
Zaburi