Link to home pageLanguagesLink to all Bible versions on this site
62
Kwa kiongozi wa muziki; Baada ya namna ya Jeduthun. Zaburi ya Daudi. 1 Katika ukimya ninamsubiri Mungu pekee; wokovu wangu watoka kwake. 2 Yeye pekee ni mwamba wangu na wokovu wangu; yeye ni mnara wangu mrefu; sitasogezwa kamwe. 3 Mpaka lini, ninyi nyote, mtamshambulia mtu, ili kwamba mumpindue yeye kama ukuta ulio inama au kama fensi isiyo imara? 4 Wanashauliana naye ili tu kumshusha chini kutoka kwenye nafasi yake heshimiwa; wao wanapenda kuongea uongo; wanambariki yeye kwa midomo yao, lakini mioyoni mwao wana mlaani yeye. Selah 5 Katika ukimya ninamsubiri Mungu pekee; kwa maana matumaini yangu yako kwake. 6 Yeye pekee ni mwamba wangu na wokovu wangu; yeye ni mnara wangu mrefu; sitasogezwa. 7 Na Mungu ni wokovu wangu na utukufu wangu; mwamba wa nguvu yangu na kimbilio langu salama liko katika Mungu. 8 Mwaminini Mungu wakati wote, ninyi watu; mimina moyo wako mbele zake; Mungu ni kimbilio salama kwa ajili yetu. Selah 9 Hakika watu wenye msimamo mdogo ni ubatili, na watu wenye msimamo mkubwa ni waongo; wao watakuwa wepesi kwenye mzani; uzito wao pamoja ni wepesi kuliko kitu chochote. 10 Usiamini katika ukandamizaji au wizi; usitumainie utajiri, maana hawatazaa matunda; usiuweke moyo wako kwenye hivyo. 11 Mungu ameongea mara moja, mara mbili nimesikia hili: nguvu ni za Mungu. 12 Pia kwako, Bwana, ni uaminifu wa agano, maana humlipa kila mtu kwa kile alichokifanya.

<- Zaburi 61Zaburi 63 ->
  • Zaburi