Link to home pageLanguagesLink to all Bible versions on this site
19
1 Kwa kiongozi wa muziki. Zaburi ya Daudi. Mbingu za tangaza utukufu wa Mungu, na mawingu hufanya kazi ya mikono yake ijulikane! 2 Siku hadi siku hotuba hutokea; usiku hadi usiku hufunua maarifa. 3 Hakuna hotuba wala misemo; sauti zao hazisikiki. 4 Bali maneno yao husambaa nje duniani kote, na hotuba zao hata mwisho wa dunia. Yeye ametengeneza hema kwa ajili ya jua kati yao. 5 Jua liko kama mfano wa bwana harusi akitokea chumbani kwake na kama mtu shujaa ambaye hushangila pale anapokimbia mbio zake. 6 Jua huchomoza kutokea upeo wa macho na likikatisha winguni kwenda jingine; hakuna chochote kinacho epuka joto lake. 7 Sheria ya Yahwe ni kamilifu, huokoa roho; ushuhuda wa Yahwe ni wa kuaminika, ukifanya hekima nyepesi. 8 Maelekezo ya Yahwe ni ya hakika, yakiufanya moyo kuwa na furaha; amri ya Yahwe ni safi, ikileta mwanga kwenye macho yetu. 9 Hofu ya Yahwe ni safi, inadumu milele; amri za haki ya Yahwe ni za kweli na zote ni za hakika! 10 Nazo zina thamani kuliko dhahabu, nazo ni tamu kuliko asali na matone ya asali kutoka sega la asali (sega la nyuki). 11 Ndiyo, kupitia hizo mtumishi wako anaonywa; na katika kuziamini kuna thawabu. 12 Ni nani ambaye aweza kuyatambua makosa yake yote mwenyewe? Unitakase makosa yaliyo fichika. 13 Pia umuepushe mtumishi wako na dhambi za majivuno; usiziruhusu kunitawala. Ndipo nitakuwa mkamilifu, na mimi sitakuwa na hatia ya makosa mengi. 14 Maneno ya midomo yangu na mawazo ya moyo wangu nayakubalike machoni pako, ewe Yahwe, mwamba wangu na mkombozi wangu.

<- Zaburi 18Zaburi 20 ->
  • Zaburi