Link to home pageLanguagesLink to all Bible versions on this site

1 Zaburi ya Daudi. Yahwe, ni nani atabaki hemani mwako? Ni nani atakaye ishi kwenye mlima wako mtakatifu? 2 Yeyote anaye tembea bila lawama, yeye hufanya kilicho haki na huongea ukweli kutoka moyoni mwake. 3 Yeye huwa hakashfu kwa ulimi wake, hawadhuru wengine, na hamtusi jirani yake. 4 Mtu asiye na maana hudharauliwa machoni pake, bali yeye huwaheshimu wale wanao mhofu Yahwe. Yeye huapa kwa hasara yake mwenyewe na habadilishi ahadi yake. 5 Yeye habadilishi nia yake aazimapo fedha. Yeye hachukui rushwa ili kumshuhudia kinyume asiye na hatia. Yeye afanyanyaye mbambo haya hatatikisika kamwe.

<- Zaburi 14Zaburi 16 ->
  • Zaburi