129
Wimbo wa kwenda hekaluni kuabudu. 1 “Mara nyingi tangu ujana wangu wamekuwa wakinishambulia,” Israeli na iseme. 2 “Mara nyingi tangu ujana wangu wamekuwa wakinishambulia, lakini hawajanishinda. 3 Wakulima wamekuwa wakilima mgonngoni kwangu; wametengeneza matuta yao marefu. 4 Yahwe ni mwenye haki; amezikata kamba za waovu.” 5 Wote waaibishwe na kurudishwa nyuma, wale wachukiao Sayuni. 6 Na wawe kama nyasi juu ya paa ambayo hunyauka kabla hayajakua, 7 ambayo hayawezi kujaza mkono wa mvunaji wala kifua cha mfunga miganda. 8 Wale wapitao karibu wasiseme, “Baraka za Mungu na ziwe juu yako; Tunakubariki katika jina la Yahwe.”
<- Zaburi 128Zaburi 130 ->
Zaburi