125
Wimbo wa kwenda hekaluni kuabudu. 1 Wale wamwaminio Yahwe ni kama mlima Sayuni, hautikisiki, wadumu milele. 2 Kama milima inavyo izunguka Yerusalemu, hivyo ndivyo Yahwe anavyo wazunguka watu wake sasa na hata milele. 3 Fimbo ya uovu haitatawala katika nchi ya wenye haki. Vinginevyo wenye haki wanaweza kukosea. 4 Ee Yahwe, utende wema kwa wale walio wema na wale walio wanyoofu mioyoni mwao. 5 Lakini kwa wale wanaogeukia njia zao za upotovu, Yahwe atawaondoa pamoja na watenda maovu. Amani iwe na Israeli.
<- Zaburi 124Zaburi 126 ->
Zaburi