124
Wimbo wa kwenda kuabudu; wa Daudi. 1 “Kama Yahwe asingekuwa upande wetu,” Israeli na aseme sasa, 2 “Kama asingekuwa Yahwe ambaye alikuwa upande wetu wakati watu walipoinuka dhidi yetu, 3 basi wangekuwa wametumeza tungali hai hasira yao lipozidi dhidi yetu. 4 Maji yangetugharikisha; mto ungetuzidia. 5 Kisha maji yafurikayo yangetuzamisha.” 6 Atukuzwe Yahwe, ambaye hajaruhusu tuwe mawindo kwa meno yao. 7 Tumetoroka kama ndege mtegoni mwa wawindaji; mtego umevunjika, nasi tumetoroka. 8 Msaada wetu uko katika Yahwe, aliyeziumba mbingu na nchi.
<- Zaburi 123Zaburi 125 ->
Zaburi