123
Wimbo wa kwenda hekaluni kuabudu. 1 Nakuinulia macho yangu, wewe uketiye mbinguni. 2 Tazama, kama vile macho ya watumishi watazamapo kwenye mkono wa Bwana wao, na kama macho ya mjakazi yatazamapo mkono wa bibi yake, ndivyo hivyo macho yetu yanamtazama Yahwe mpaka atakapo tuhurumia. 3 Ee Yahwe, utuhurumie, kwa maana tunadhalilishwa sana. 4 Tumeshibishwa mzaha wa wenye kiburi na dharau ya wenye majivuno.
<- Zaburi 122Zaburi 124 ->
Zaburi