Obadia
1 Maono ya Obadia. Bwana MUNGU asema hivi juu ya Edomu Tumesikia habari kutoka kwa Bwana, na mjumbe ametumwa kati ya mataifa, akisema, Inukeni! Tuinuke dhidi yake kwa vita!” 2 Tazama, nitawafanya wadogo kati ya mataifa, mutadharauliwa sana. 3 Kiburi cha moyo wako kimekudanganya wewe, wewe ambaye unishi katika makaburi ya miamba, katika nyumba yako ya juu; asemaye moyoni mwako, 'Ni nani atakayenishusha mimi chini?' 4 Ingawa unasimama juu kama tai na ingawa kiota chako huwekwa kati ya nyota, nitakushusha chini kutoka huko, asema Yahweh. 5 Kama wezi walikuja kwako, ikiwa wanyang'anyi wangekujilia usiku (jinsi ungekatilwa mbali!), Wasingeweza kuiba vya kuwatosha? Ikiwa wakusanya zabibu wangekujilia, wasingeacha mavuno? 6 Jinsi Esau amekwisha kupigwa, na hazina zake zilizofichwa zimewekwa nje! 7 Watu wote wa ushirikiano wako watakupeleka katika njiani ya hadi mpakani. Watu waliokuwa na amani pamoja nawe wamekudanganya, na kukushinda. Wale wanaokula mkate wako wameweka mtego chini yako. Hakuna uelewa ndani yake. 8 Je! Sikuweza siku hiyo, asema Bwana, kuwaangamiza watu wenye hekima kutoka Edomu na kuelewa kutoka mlima wa Esau? 9 Mashujaa wako watafadhaika, Temani, ili kila mtu akatiliwe mbali kutoka mlima wa Esau kwa kuuawa. 10 Kwa sababu ya ukatili uliofanywa kwa ndugu yako Yakobo, utafunikwa na aibu, nawe utakatiliwa mbali milele. 11 Siku ile ulikuwa umesimama, siku wageni walichukua mali zake, na waliokuwa wageni katika malango yake, na kupiga kura kwa Yerusalemu, wewe ulikuwa kama mmoja wao. 12 Lakini usifurahi siku ya ndugu yako, siku ya msiba wake, wala usifurahi juu ya watu wa Yuda siku ya uharibifu wao; msijisifu siku ya dhiki yao. 13 Usiingie mlango wa watu wangu siku ya msiba wao; usifurahi juu ya taabu yao siku ya msiba wao, wala msipotee utajiri wao siku ya uharibifu wao. 14 Usisimama kwenye njia panda, ili kuwakatilia mbali wakimbizi wake na usiwatoe waathirika wake katika siku ya dhiki. 15 Kwa maana siku ya Bwana iko karibu na mataifa yote. Kama ulivyofanya, itafanyika kwako; matendo yako yatarudi juu ya kichwa chako mwenyewe. 16 Kwa vile mlivyokunywa katika mlima wangu mtakatifu, ndivyo mataifa yote yatakavyo kunywa daima. Watakunywa na kumeza na itakuwa kana kwamba hawakuwepo kabisa. 17 Lakini katika Mlima Sayuni kutakuwa na wale waliookoka na watakuwa watakatifu; na nyumba ya Yakobo watamiliki miliki zao. 18 Nyumba ya Yakobo itakuwa moto, na nyumba ya Yusufu ni mwali wa moto, na nyumba ya Esau itakuwa mabua makavu, nao watawaunguza, na kuwateketeza. Hakutakuwa na waathirika kwa nyumba ya Esau, kwa kuwa Bwana amesema. 19 Wote kutoka Negebu watamiliki mlima wa Esau na wale wa Shepela watamiliki nchi ya Wafilisti. Wao wataimiliki nchi ya Efraimu na nchi ya Samaria; na Benyamini atamiliki Gileadi. 20 Wahamiaji wa jeshi hili la watu wa Israeli watamiliki ardhi ya Kanaani mpaka Sarepta. Wahamiaji wa Yerusalemu, waliopo Sefaradi, wataimiliki miji ya Negebu. 21 Waokoaji watakwenda hadi juu ya Mlima Sayuni kutawala nchi ya vilima ya Esau, na ufalme utakuwa wa Bwana.