Link to home pageLanguagesLink to all Bible versions on this site
36
1 Kisha wale viongozi wa nyumba za mababa wa ukoo wa Gileadi mwana wa Machiri (ambaye alikuwa mwana wa Manase), ambao walikuwa wa ukoo wa uzao wa Yusufu, walikuja wakasema mbele za Musa na mbele za vionigozi wa familia za mababa wa watu wa Israeli. 2 Wakasema, “BWANA alikuamuru, wewe bwana wetu, kutupa mgawo wa ardhi kwa kura kwa wana wa Israeli. Uliamuriwa na BWANA kutoa mgawo wa Zerofehadi kaka yetu kwa binti zake. 3 Lakini hawa binti wameolewa na wanaume toka kabila zingine za wana wa Israeli, basi mgawo wao wa ardhi utaondolewa kutoka kwenye mgawo wa mababa zao. Utaongezwa kwenye mgawo wa makabila ambayo wao wanaungana nao. Kwa sababu hiyo, Utaondolewa kwenye mgawo uliopangwa kwenye urithi wetu. 4 Kwa sababu hiyo, wakati wa mwaka wa yubilee ya wana wa Israeli utakapofika, mgawo wao utaunganishwa na kabila ile waliyoungana nao. Kwa sababu hii mgawo wao utaondolewa kwenye mgawo wa mababa zetu.” 5 Basi Musa akawapa amri wana wa Israeli, kwa neno la BWANA. Akasema, “Kile wanachosema watu wa kabila la Yusufu kiko sahihi. 6 Hiki ndicho BWANA anaagiza kuhusu mabinti wa Zelofehadi. Anasema, 'Acha waolewa na wale ambao wao wanaofikri ni vizuri zaidi, lakini lazima waolewe ndani ya kabila ya baba yao.' 7 Hakuna mgawo wa watu utakaobadilika kutoka kabila moja kwenda jingine. Kila mtu wa Israeli ataendelea na mgawo wa kabila ya baba y ake. 8 Kila mwanamke wa watu wa Israeli aliye na mgao kwenye kabila lake lazima aolewe na mtu wa ukoo unaotoka kwenye kabila la baba yake. Hii itafanyika hivyo ili kila mtu wa wana wa Israeli aweze kuwa na urithi kutoka kwa mababa zake. 9 Hakuna mgawo utakaobadilika kutoka kabila nyingine kwenda kabila nyingine. Kila mtu wa kabila za watu wa Israeli atalinda urithi wake.” 10 Kwa hiyo wale binti wa Zelofehadi walifanya kama vile BWANA alivyokuwa amemwamuru Musa. Mahila, Tiriza, Hogila, Milika, na Noha, binti za 11 Zelofehadi, waliolewa na wana wa uzao wa Manase. 12 Waliolewa katika koo za uzao wa Manase mwana wa Yusufu. Kwa sababu hii, urithi wao ulibaki kwenye kabila la ukoo ambalo baba yao alikuwa anatoka. 13 Hizi ndizo amri na maagizo ambayo BWANAaliyatoa kupitia Musa kwa wana wa Israeli katika nyanda za Moabu karibu na Yorodani huko Yeriko.

<- Hesabu 35
  • Hesabu