1 Yeyote akitoa sadaka ya nafaka kwa Bwana, sadaka yake lazima iwe unga safi, na atamwaga mafuta juu yake na kuweka ubani juu yake. 2 Atachukua sadaka kwa wana wa Haruni, makuhani na pale kuhani atachukua konzi moja ya unga safi pamoja na mafuta na ubani. Kisha kuhani atateketeza hiyo sadaka juu ya madhabahu kuwa shukrani kwa uzuri wa Bwana. Italeta harufu nzuri sana kwa Bwana, itakuwa sadaka ya Bwana iliyotolewa kwa moto. 3 Unga wowote uliobaki utakuwa ni wa Haruni na watoto wake. Ni takatifu sana kwa Bwana iliyotolewa sadaka kwa Bwana kwa moto. 4 Kisha utakapotoa sadaka ya unga bila chachu iliyookwa kweye kiokeo, itakuwa mkate lainiya unga safi uliochanganywa na mafuta, au mkate mgumu usiokuwa na chachu, ambao umesambazwa na mafuta. 5 Kama matoleo yako ya nafaka yameokwa na kikaango cha chuma ni lazima iwe unga safi bila chachu uliochanganywa na mafuta. 6 Utagawanya katika vipande na kumwaga mafuta juu yake. Hii ni sadaka ya nafaka. 7 Kama sadaka yako ya nafaka imepikwa katika kikaango, ni lazima iwe imetengenezwa kwa unga safi na mafuta. 8 Utaleta matoleo ya nafaka yaliyotengenezwa kwa vitu hivi kwa Bwana, italeta kwa kuhani, ambaye ataleta mbele ya madhabahu. 9 Ndipo kuhani atachukua baadhi ya sadaka ya nafaka ya shukrani ya Bwana, ataitekeza katika madhabahu. Itakuwa sadaka ya kuteketezwa kwa moto, italeta harufu nzuri kwa Bwana. 10 Itakayobaki sadaka ya nafaka itakuwa ya Haruni na wanawe. Itakuwa takatifu kamili ya Bwana kutoka matoleo kwa Bwana yatolewayo kwa moto. 11 Sadaka ya nafaka itolewayo kwa Bwana isiwe na chachu, hautatekeza chachu wala asali kama matoleo yatakayotekezwa kwa moto kwa ajili ya Bwana. 12 Utayatoa kwa Bwana kama mazao ya kwanza, lakini hayatatumika kama matoleo ya harufu nzuri ya moto juu ya madhabahu. 13 Utaweka chumvi katika kila matoleo yako ya nafaka. Usipungukie chumvi ya agano la Bwana katika matoleo yako ya unga. Matoleo yako yote hayatapungukiwa na chumvi. 14 Kama ukitoa matoleo ya nafaka ya mazao ya kwanza kwa Bwana, utatoa nafaka mbichi yaliyookwa kwa moto, na yaliyopondwa. 15 Lazima utaweka mafuta na ubani juu yake. Haya ni matoleo ya nafaka. 16 Kuhani atatoa sehemu ya nafaka iliyopondwa na mafuta na ubani, kama sadaka ya shukrani itolewayo kwa uzuri wa Bwana. Hii ni sadaka ya Bwana inayotolewa kwa moto.
<- Mambo ya Walawi 1Mambo ya Walawi 3 ->