Link to home pageLanguagesLink to all Bible versions on this site
17
1 Roho yangu imemezwa, na siku zangu zimekwisha; kaburi lipo tayari kwa ajili yangu mimi. 2 Hakika kuna wenye mzaha pamoja nami; ni lazima daima jicho langu litazame kukasirisha kwao. 3 Nipe sasa ahadi, uwe uthibitisho kwangu mimi pamoja na wewe mwenyewe; nani mwingine yuko pale ambaye atanisaidia mimi? 4 Kwa kuwa wewe Mungu umemeitunza mioyo yao kutoka katika ufahamu; kwa hiyo, wewe hautawaheshimisha wao juu yangu mimi. 5 Yeye ambaye huwapinga rafiki zake hadharani, kwa ajili ya tuzo, macho ya watoto wake yatashindwa kuona. 6 Lakini amenifanya mimi kuwa neno la kuzungumziwa na watu; wao wananitemea mate katika uso wangu mimi. 7 Jicho langu pia halioni vizuri kwa sababu ya huzuni; sehemu zangu zote za mwili ni nyembamba kama vivuli. 8 Watu wanyoofu watapendezwa na hiki; mtu asiye na hatia atajitia yeye mwenyewe juu ya kushindana dhidi ya watu wasiomcha Mungu. 9 Mtu mwenye haki ataendelea katika njia yake; yeye ambaye ana mikono iliyo safi ataendelea kuwa mwenye nguvu zaidi na zaidi. 10 Lakini kama ilivyo kwenu ninyi nyote, njooni sasa; Mimi sitampata mtu mwenye hekima miongoni mwenu ninyi. 11 Siku zangu zimepita; mipango yangu imenyamazishwa na hivyo ni matumaini ya moyo wangu. 12 Watu hawa, wenye kukejeli, badili usiku kuwa mchana; mchana uko karibu kuwa giza. 13 Tangu mimi nitazame katika Kuzimu kama nyumbani kwangu; tangu Mimi nimetandaza kiti changu katika giza; 14 tangu Mimi nimesema na shimo 'Wewe ni baba yangu,' na kwa funza, 'Wewe ni mama yangu au dada yangu; 15 liko wapi tena tumaini langu? Kama kwa tumaini langu, nani awezaye kuona chochote? 16 Tumaini litakwenda pamoja na mimi katika milango ya Kuzimu wakati sisi tutakapokwenda katika mavumbi?

<- Ayubu 16Ayubu 18 ->
  • Ayubu