1 Wanaema, 'Mwanamume akimfukuza mke wake, naye akaondoka kwake na kuwa mke wa mwanamume mwingine. Je, anaweza kumrudia tena? Je huyo si najisi kabisa?' Huyo mwanamke ndiyo hii nchi! Mmetenda kama kama Kahaba aliye na wapenzi wengi, na sasa mnapenda kurudi kwangu tena? - asema BWANA wa majeshi. 2 Inua macho yako uvitazame vielele tasa! Je kuna mahali ambapo hukufanya ukahaba? Pembeni mwa barabara ulikaa ukisubiri wapenzi wako, kama vile Mwarabu jangwani. Uneiharibu nchi kwa ukahaba na uovu wako. 3 Kwa hiyo chemichemi za mvua zilizuiliwa na mvua za vuli hazikunyesha. Lakini uso wako una kiburi, kama uso wa mwanamke kahaba. Unakataa kuona aibu. 4 Na sasa hutaniita mimi: 'Baba yangu, hata marafiki zangu wa tangu ujanani! Je, atakuwa na hasira dhidi yangu milele? 5 Je, utaendelea kuwa na hasira zako?' Tazama! Umesema kuwa utatenda maovu, na kweli umetenda hivyo. kwa hiyo endelea kufanya hivyo!” 6 Kisha BWANA akanena nami katika siku za mfalme Yosia, “Je, unaona jinsi Israeli alivyoniasi? Yeye anaenda kwenye kila kilima na katika kila mti wenye majani mabichi, na kule anafanya kama mwanamke kahaba. 7 Nikisema, 'Baada ya kuwa amefanya mambo haya yote, atanirudia,' lakini hakurudi. Kisha dada yake Yuda ambaye ni mwasi pia aliona alichokifanya. 8 Kwa hiyo nami nikaona kuwa kwa sababu amefanya uzinzi huu wote. Huyo Israeli aliyeasi! Nilimfukuza na kumpatia talaka ya ndoa. Lakini dada yake Yuda mwenye hiana hakuwa na hofu, na yeye akaenda kuafanya kama mwanamke kahaba! 9 Hukusikitika kuwa ameinajisi nchi, kwa hiyo wakatengeneza sanamu za mti na za jiwe. 10 Kisha baada ya haya yote, wala Yuda dada yake muasi hakurudi kwangu na moyo wake wote, bali alikuja na uongo! -asema BWANA wa majeshi,” 11 Kisha BWANA akanena na mimi, “Israeli muasi amekuwa mwenye haki zaidi kuliko Yuda muasi! 12 Nenda ukaseme maneno haya huko kaskazini. Uwaambie, 'Rudi wewe Israeli uliyeasi! - asema BWANA - sitakuwa na hasira dhidi yako. Kwa kuwa mimi ni mwaminifu - asema BWANA - sitakuwa na hasira milele. 13 Kiri uovu wako, kwa kuwa umefanya dhambi dhidi ya BWANA, Mungu wako; umemshirikisha njia zako mgeni chini ya kila mti wenye majani mabichi! wala hukuisikiliza sauti yangu! - asema BWANA. 14 Rudini, enyi watu waasi! - asema BWANA - kwa kuwa mimi nimekuoa wewe! Nitakurudisha wewe mmoja katika mji, wawili katika ukoo mmoja, na nitawarudisha Sayuni! 15 Nitawapa wachungaji niwapendao, na watawachunga kwa maarifa na ufahamu. 16 Ndipo itakapotokea kuwa utaongezeka na kuzaa matunda katika nchi hiyo siku hizo-asema BWANA. Hawataweza kusema kuwa, “Sanduku la agano la BWANA! Jambo hili hawatalikumbuka tena katika mioyo yao, kwa kuwa hawataliwaza tena wala kulijali tena. Usemi huu hawatausema tena.' 17 Katiak wakati huo watasema juu ya Yerusalemu, 'Hii ndiyo enzi ya BWANA,' na mataifa mengine yote yatakusanyika Yerusalemu katika jna la BWANA. Hawataishi katika taabu ya uovu wa mioyo yao. 18 Katika siku hizo, nyumba ya Yuda itaishi na nyumba ya Israeli. Watarudi pamoja kutoka katika nchi ya kaskazini katika nchi niliyowapa mababu wao kuwa urithi. 19 Lakini mimi, Nilisema, 'Jinsi nipendavyo kukuheshimu kama mwanangu na kukupa nchi ipendezayo, kuwa urithi mzuri kuliko ulio katika taifa lolote!' Nami nikasema, ''mtaniita baba yangu''.'Nami nitasema kwamba hamtageuka na kuacha kunifuata. 20 Lakini kama mwanamke aliyemwasi mume wake, mmenisaliti, enyi nyumba ya Israeli - asema BWANA.” 21 Sauti ilisikika juu ya nyanda, kilio na kusihi kwa watu wa Israeli! kwa kuwa wamezibadili njia; wamemsahau BWANA, Mungu wao. 22 “Rudini enyi watu mlioasi! Nami nitawaponya na uasi wenu!” “Tazama! tutakuja kwako, kwa kuwa wewe ni BWANA, Mungu wetu! 23 Uongo hutoka kwenye vilima, kutoka kwenye milima mingi. Kwa hakika wokovu wa Israeli unapatikana kwa BWANA, Mungu wetu. 24 Lakini miungu ya aibu imeramba kazi ambayo mababu zetu waliifanya - makundi yao ya kondoo na ng'ombe, wana wao na binti zao! 25 Na tulale chini kwa aibu. Aibu yetu na itufunike, kwa kuwa tumefanya dhambi dhidi ya BWANA, Mungu wetu! Sisi wenyewe na mababu zetu, kutoka wakati wa ujana wetu hadi leo, hatujaisikiliza sauti ya BWANA, Mungu wetu!”
<- Yeremia 2Yeremia 4 ->