46
1 Bwana Yahwe asema hivi: Lango la uzio wa ndani, linaloelekea mashariki, litafungwa kwa mda wa siku sita za kazi, lakini katika siku za Sabato litakuwa wazi, na katika siku ya mwezi mpya litafunguliwa. 2 Mwana wa mfalme ataingia kwa kutumia lango la njia ya nyuma ya varanda upande wa nje, na atasimama mbele ya muhimili wa mwimo wa lango la ndani wakati makuhani wakiwa wakitengeza sadaka ya kuteketezwa na sadaka ya amani. Kisha ataabudu kwenye kizingiti cha lango la ndani na kutoka nje, lakini lango halitakuwa linafungwa hadi jioni. 3 Watu wa nchi pia wataabudu mbele ya Yahwe kwenye hili lango la kuingilia katika siku ya Sabato na siku mpya za mwezi. 4 Sadaka ya kuteketezwa ambayo mwana wa mfalme aitoayo kwa Yahwe katika siku ya Sabato itakuwa wanakondoo sita wasiokuwa na dosari na kondoo dume asiyekuwa na dosari. 5 Sadaka ya unga pamoja na kondoo dume itakuwa efa moja, na sadaka ya unga pamoja na wanakondoo kiasi awezacho kutoa, na hini moja ya mafuta pamoja na kila efa ya unga. 6 Katika siku ya mwezi mpya atatoa ng'ombe mchanga asiyekuwa na dosari kutoka kuchungwa, wanakondoo sita, na kondoo asyekuwa na dosari. 7 Atatengeneza sadaka ya unga ya efa moja kwa ajili ya ng'ombe na efa moja kwa ajili ya kondoo, na kwa kiasi awezacho kukitoa kwa ajili ya wanakondoo, na hini ya mafuta kwa kila efa ya unga. 8 Wakati mwana wa mfalme atakapokuwa anaingia kwa njia ya lango lenye varanda, ataondoka kwa njia hiyo hiyo. 9 Lakini wakati watu wa nchi watakakuja kwa Yahwe katika sikukuu zilizoteuliwa, kila mmoja kuingia kupitia kwenye lango la kaskazini kuabudu ataondoka kupitia lango la kusini; na kila atakayeingillia kupitia lango la kusini atatoka kupitia lango la kaskazini. Hakuna atakayerudia kwa lile lango aliloingilia, kwa kuwa atatoka nje moja kwa moja. 10 Mwana wa mfalme atakuwa kati yao; watakapoingia, ataingia ndani, na watakapoondoka, atatoka nao. 11 Kwenye sikukuu hizo, sadaka ya unga itakuwa efa moja ya unga kwa ng'ombe mmoja na efa moja kwa kondoo dume, na chochote atakacho kitoa pamoja na wanakondoo, na hini moja ya mafuta kwa kila efa. 12 Wakati mwana wa mfalme atakapotoa sadaka atakayojisikia kutoa, labda sadaka ya kuteketezwa au sadaka ya amani kwa Yahwe, lango la kuelekea mashariki litafunguliwa kwa ajili yake. Atatoa sadaka yake ya kuteketezwa au sadaka ya amani kama afanyavyo siku ya Sabato. Kisha atatoka nje, na baada ya kutoka lango litafungwa. 13 Kwa kuongeza, utatoa mwanakondoo asiyekuwa na dosari mwenye umri wa mwaka mmoja kama sadaka ya kuteketezwa kwa Yahwe kila siku; utafanya hivi kila asubuhi. 14 Utatoa sadaka ya unga pamoja nayo kila asubuhi, efa sita na sehemu ya tatu ya hini ya mafuta kuchanganya na sadaka ya unga kwa ajili ya Yahwe, kulingana na sheria ilivyo. 15 Watandaa mwanakondoo, sadaka ya kuteketezwa, na mafuta kila asubuhi, sadaka ya kuteketezwa ya kudumu. 16 Bwana Yahwe asema hivi: Kama mwana wa mfalme akitoa zawadi kwa mmoja wa watoto wake, imekuwa urithi wake. Itakuwa mali ya mtoto wake, imekuwa urithi. 17 Lakini kama akimpatia zawadi kutoka urithi wake kwa mmoja wa watumishi wake, kisha itakuwa ya huyo mtumishi mpaka mwaka wa uhuru, na kisha itarudi kwa mwana wa mfalme. Urithi wake yamkini ukawa kwa ajili ya watoto wake. 18 Mwana wa mfalme hatawaondolea urithi wa watu kutoka kwenye mali zao wenyewe; ataandaa kwa ajili ya watoto wake mali ili kwamba watu wangu wasitawanyike, kila mtu kutoka mali kwenye yake mwenyewe.” 19 Kisha yule mtu akaniletea kwenye lango la kutokea hata kwenye vyumba vitakatifu kwa ajili ya makuhani, vilivyokuwa vimeelekea kaskazini na tazama! Kulikuwa na sehemu mbele magharibi. 20 Akanambia, “Hii ndio sehemu ambayo makuhani watakapo chemshia sadaka ya hatia na sadaka ya dhambi na walipookea sadaka ya unga. Wasilete sadaka nje ya uzio, kwa kuwa watu watatakaswa.” 21 Kisha akanileta kwenye uzio wa nje akaniongoza kuzunguka pembe nne za uzio, nikaona kwamba katika kila pembe ya uzio kulikuwa na uwanja. 22 Katika hizo pembe nne za nje ya uzio kulikuwa na nzio nne ndogo, dhiraa arobaini urefu na thelathini upana. Ukubwa ule ule kwa nzio zote nne. 23 Kulikuwa na safu zilizokuwa zimetengenezwa kwa mawe kuzizunguka zote nne, na meko ya kupikia ilikuwa chini ya safu ya jiwe. 24 Yule mtu akanambia, “Hizi ndizo sehemu ambazo watumishi watachemshia dhabihu za watu.”
<- Ezekieli 45Ezekieli 47 ->
Ezekieli