10
1 Malkia wa Sheba aliposikia uvumi wa Sulemani kuhusu jina la BWANA, alikuja kumjaribu kwa maswali magumu. 2 Alikuja Yerusalemu na msafara mrefu, pamoja na ngamia waliokuwa wamebeba mizigo ya manukato, dhahabu nyingi, na mawe mengi ya thamani, akamwambia Sulemani yote yaliyokuwa moyoni mwake. 3 Sulemani akajibu maswali yake yote. Hapakuwepo na swali ambalo aliuliza na mfalme akashindwa kujibu. 4 Malkia wa Sheba alipoona hekima yote ya Sulemani, na ikulu aliyokuwa amejenga, 5 chakula cha mezani kwake, kuketi kwa watumishi wake, kazi ya watumishi wake na kuvaa kwao, pia wanyweshaji wake, na jinsi alivyotoa sadaka za kuteketezwa katika nyumba ya BWANA, roho yake ilizimia. 6 Akamwambia mfalme, “Ni kweli, ile taarifa ambayo nimeisikia nchini kwangu juu ya maneno yako na hekima yako. 7 Sikuamini kile nilichosikia hadi nilipofika hapa, na sasa macho yangu yamejionea. Hata nusu ya hekima na utajiri wako! Umezidi uvumi ambao nilikuwa nimesikia. 8 Tazama jinsi walivyobarikiwa wake zako, na jinsi walivyobarikwa watumishi wako ambao daima husimama mbele yako, kwa sababu wanasikia hekima zako. 9 BWANA, Mungu wako asifiwe, ambaye amependezwa na wewe, ambaye alikuweka kwenye kiti cha enzi cha Israeli. Kwa sababu BWANA aliipenda Israeli milele, na sasa amekufanya wewe kuwa mfalme, ili kwamba utoe hukumu ya kweli na ya haki. 10 Basi Malikia alimpatia mfalme zaidi ya kilo 4500 za dhahabu na kiasi kikubwa cha mawe ya thamani. Hapakuwahi kutokea kiasi kikubwa cha viungo kama hiki ambacho Malkia wa Sheba alitoa kwa mfalme Sulemani kuwahi kutolewa tena. 11 Ile merikebu ya Hiramu, ambayo ilileta dhahabu kutoka Ofri, pia ilileta Kutoka Ofri kiasi kikubwa cha miti ya msandali na vito vya thamani. 12 Mfalme alitengeneza nguzo za hekalu kwa ajili ya hekalu la BWANA na kwa nyumba ya mfalme, na vinubi na vinanda kwa hao waimbaji. haijatokea kiasi cha miti ya misandali kama hicho ambacho kimewahi kutokea hadi leo. 13 Mfame Sulemani alimpatia Malkia wa Sheba kila kitu ambacho alihitaji, na kila kitu alichoomba, na zaidi ya yote Sulemani alimpatia kwa ukarimu wake vitu vya kifalme. Kisha akarudi kwake na watumishi wake. 14 Kiasi cha dhahabu ambazo zililetwa kwa Sulemani kwa mwaka mmoja kilikuwa takribani kilo elfu ishirini na tatu za dhahabu, 15 zaidi ya dhahabu ambazo wafanya biashara na wachuuzi walileta. Wafame wote wa Uarabuni na maliwali wa nchi pia walileta dhahabu na fedha kwa Sulemani. 16 Mfalme Sulemani alitengeneza ngao mia mbili za dhahabu iliyofuliwa, shekeli mia sita za dhahabu zilichukuliwa pamoja na ngao. 17 Pia alitengeneza ngao mia tatu za dhahabu iliyofuliwa. Mane tatu za dhahabu ziliambatana pamoja na ngao moja moja; mfalme aliviweka katika ikulu ya mwitu ya Lebanoni. 18 Kisha mfalme akafanya kiti kikubwa cha enzi kwa pembe na akakisakafia kwa dhahabu laini. 19 Hicho kiti kilikuwa na ngazi sita, na kitako chake kilikuwa cha mviringo. Na kilikuwa kimezungushiwa kwa mikono pande zake zote. Na simba wawili walisimama pembeni mwa ile mikono. 20 Kulikuwa na simba kumi na wawili waliokuwa wamesimama kwenye ile ngazi. Moja katika kila upande wa ngazi hizo. Hapakuwepo na kiti kama hicho katika ufalme mwingine. 21 Vikombe vyote vya kunywea vya mfalme Sulemani vilikuwa vya dhahabu. Na vikombe vyote vya kunywea vya ikulu ya mwitu wa Lebanoni vilikuwa vya dhahabu safi. Hapakuwepo na kikombe cha fedha, kwa sababu fedha haikuwa na thamani katika siku za Sulemani. 22 Mfalme alikuwa na merikebu za kusafiri pamoja na merikebu za Hiramu. Mara moja kila mwaka merikebu zilileta dhahabu, fedha, na pembe za ndovu, pamoja na nyani na tumbili. 23 Kwa hiyo mfalme Sulemani aliwazidi wafalme wote ulimwenguni katika utajiri n a hekiima. 24 Dunia yote ilitafuta uwepo wa Sulemani ili kusikia hekima yake, ambayo Mungu alikuwa ameweka katika moyo wake. 25 Na wote waliomtembelea walilipa Kodi, vyombo vya fedha na vya dhahabu, na nguo na manukato na silaha na farasi na nyumbu, mwaka baada ya mwaka. 26 Sulemani alikusanya pamoja magari n a wapanda farasi. Alikuwa na magari 1, 400 na wapanda farasi elfu kumi na mbili ambao alikuwa amewaweka kwenye miji ya magari pamoja naye Yerusalemu. 27 Mfalme alikuwa na fedha kule Yerusalemu, pamoja na mawe ardhini. Alitengeneza miti ya mierezi kuwa mingi kama mikuyu iliyo katika nyanda za chini. 28 Sulemani alimiliiki farasi waliokuwa wamenunuliwa kutoka Misri na Kilikia. Wachuuzi wa mfalme waliwanunua kwa makundi, kila kundi kwa bei yake. 29 Magari yalinunuliwa kutoka Misri kwa shekeli mia sita za fedha kila moja, na farasi kwa shekeli 150 kila moja. Vitu vingi katika hivi baadaye viliuzwa kwa wafalme wote wa Wahiti na Aramu.
<- 1Wafalme 91Wafalme 11 ->
1Wafalme