Link to home pageLanguagesLink to all Bible versions on this site
16
1 Sasa kuhusu michango kwa ajili ya waumini, kama nilivyo elekeza makanisa ya Galatia, vivyo hivyo mwapaswa kufanya. 2 Katika siku ya kwanza ya wiki, kila mmoja wenu aweke kitu fulani kando na kukihifadhi, kama muwezavyo. Fanyeni hivyo ili kwamba kusiwe na michango wakati nikija. 3 Na nitakapofika, yeyote mtakayemchagua, nitamtuma pamoja na barua kutoa sadaka yenu huko Yerusalem. 4 Na kama ni sahihi kwa mimi kwenda pia, watakwenda pamoja nami. 5 Lakini nitakuja kwenu, wakati ninapitia Makedonia. Kwa kuwa nitapitia Makedonia. 6 Labda naweza kukaa nanyi au hata kumaliza majira ya baridi, ili kwamba muweze kunisaidia katika safari yangu, popote niendako. 7 Kwa kuwa sitarajii kuwaona sasa kwa muda mfupi. Kwani ninatumaini kukaa nanyi kwa muda fulani, kama Bwana ataniruhusu. 8 Lakini nitakaa Efeso mpaka Pentekoste, 9 kwa kuwa mlango mpana umefunguliwa kwa ajili yangu, na kuna maadui wengi wanipingao. 10 Sasa wakati Timotheo akija, muoneni kwamba yuko na ninyi pasipo kuogopa, anafanya kazi ya Bwana, kama ninavyofanya. 11 Mtu yeyote asimdharau. Mumsaidie katika njia yake kwa amani, ili kwamba aweze kuja kwangu. Kwa kuwa ninamtarajia aje pamoja na ndugu. 12 Sasa kuhusiana na ndugu yetu Apolo. Nilimtia moyo sana kuwatembelea ninyi pamoja na ndugu. Lakini aliamua kutokuja kwa sasa. Hata hivyo, atakuja wakati ana nafasi. 13 Muwe macho, simameni imara, mtende kama wanaume, muwe na nguvu. 14 Basi yote myafanyayo yafanyike katika upendo. 15 Mnaijua kaya ya Stefana. Mnajua kwamba walikuwa waamini wa kwanza huko Akaya, na kwamba walijiweka wenyewe kwenye huduma ya waumini. Na sasa nawasihi, kaka na dada zangu, 16 kuweni wanyenyekevu kwa watu kama hao, na kwa kila mtu anayesaidia katika kazi na watenda kazi pamoja nasi. 17 Na ninafurahi kwa ujio wa Stefana, Fotunato, na Akiko. Wamesimama mahali ambapo ninyi mgepaswa kuwa. 18 Kwa kuwa wameifurahisha roho yangu na yenu. Kwa hiyo sasa, watambueni watu kama hawa. 19 Makanisa ya Asia wametuma salamu kwenu. Akila na Priska wanawasalimu katika Bwana, pamoja na kanisa lililoko nyumbani kwao. 20 Kaka na dada zangu wote wanawasalimu. Salimianeni kwa busu takatifu. 21 Mimi, Paulo, naandika hivi kwa mkono wangu. 22 Kama yeyote hampendi Bwana, basi laana iwe juu yake. Bwana wetu, njoo! 23 Neema ya Bwana Yesu iwe nanyi. 24 Upendo wangu uwe pamoja nanyi katika Kristo Yesu.

<- 1 Wakorintho 15
  • 1 Wakorintho