26
1 Huu ulikuwa mgawanyiko wa walinzi wa lango: Kutoka kwa Wakora, Meshelemia mwana wa Kore, wa uzao wa Asafu. 2 Meshelemia alikuwa na wana wa kiume: Zekaria mzaliwa wa kwanza, Yediaeli wapili, Zebadia watatu, Yathinieli wanne, 3 Elamu watano, Yehohanani wasita, Eliehoenai wasaba. 4 Obedi alikuwa na wana wa kiume: Shemaia wa kwanza, Yehozabadi wapili, Yoa watatu, na Sakari wanne, na Nethanieli watano, 5 Amieli wasita, Isakari wasaba, Peulethai wanane, kwa kuwa Mungu alimbariki Obedi Edomu. 6 Kwa Shemaia mwanae walizawa wana walio tawala familia zao; walikuwa wanaume wenye uwezo mbali mbali. 7 Wana wa Shemaia walikuwa Othini, Refaeli, Obedi, na Elizabadi. Ndugu zake Elihu na Semakia walikuwa wanaume wenye uwezo mbali mbali. 8 Hawa wote walikuwa uzao wa Obedi Edomu. Wao na wanao na ndugu zao walikuwa wanaume wenye uwezo wa kufanya wajibu wao katika huduma ya hema la kuabudia. Palikuwa na sitini na mbili walio kuwa na undugu na Obedi Edomu. 9 Meshelemia alikuwa na wana na ndugu, wanaume wenye uwezo, jumla ya kumi na nane. 10 Hosa, mzao wa Merari, alikuwa na wana: Shimiri kiongozi (japo hakuwa mzaliwa wa kwanza, baba yake alimfanya kiongozi), 11 Hilikia wapili, Tebalia watatu, Zekaria wanne. Wote wa wana wa Hosa na ndugu walikuwa kumi na tatu kwa idadi. 12 Huu mgawanyiko wa walinzi wa lango, sambamba na viongozi, ulikuwa na majukumu, kama ndugu zao, kutumika katika nyumba ya Yahweh. 13 Walirusha kura, wadogo kwa wakubwa, kulingana na familia zao, kwa kila lango. 14 Kura ilipo rushwa kwa lango la mashariki, ilimuangukia Shelemia. Kisha wakarusha kura kwa Zekaria mwana wake, mshauri makini, na kura yake ikatokea lango la kaskazini. 15 Kwa Obedi Edomu kulipangiwa lango la kusini, na wanae walipangiwa nyumba za ghala. 16 Shufimu na Hosa walipangiwa lango la magharibi pamoja na lango la Shalekethi, kwa barabara ya juu. Lindo lilikabiidhiwa kwa kila familia. 17 Kwa mashariki walikuwa Walawi sita, kaskazini kwa siku moja, kusini kwa siku moja, na nyumba za ghala wawili. 18 Katika ua kuelekea magharibi wanne walipangwa, wanne barabarani, na wawili katika ua. 19 Haya yalikuwa magawanyiko ya walinzi wa lango. Palijazwa na uzao wa Kora na Merari. 20 Miongoni mwa Walawi, Ahija alikuwa kiongozi wa hazina ya nyumba ya Mungu, na hazina ya vitu vya Yahweh. 21 Wazao wa Ladani, walitoka kwa Gerishoni kupitia kwake na walio kuwa viongozi wa familia za Ladani Mgerishoni, walikuwa Yehieli na wanae, 22 Zethamu, na Yoeli kaka yake, aliyesimamia ghala za nyumba ya Yahweh. 23 Kulikuwa na askari walio chukuliwa kwa koo za Amramu, Izhari, Hebroni, na uzieli. 24 Shebueli mwana wa Gerishomu mwana wa Musa, alikuwa msimamizi wa nyumba za ghala. 25 Ndugu zake wa ukoo wa Eliezeri walikuwa Rehabia mwanae, mwana wa Rehabia Yeshaia, mwana wa Yeshaia Yoramu, mwana wa Yoramu Zikiri, na mwana wa Zikiri Shelomothi. 26 Shelomothi na ndugu zake walikuwa wasimamizi wa nyumba zote za ghala zinazo hifadhi vitu vyote vya Yahweh, ambavyo Daudi mfalme, viongozi wa familia, wakuu wa maelfu na mamia, na wakuu wa jeshi walivyo vitenga. 27 Walitenga vitu walivyo vichukuwa kwenye mapambano kwa ajili ya kutunza nyumba ya Yahweh. 28 Pia walikuwa wahusika wa kila kitu kilicho tengwa kwa ajili ya Yahweh na Samweli nabii, Sauli mwana wa Kishi, Abneri mwana wa Neri, na Yoabu mwana wa Zeruia. Kila kitu kilicho tengwa kwa ajili ya Yahweh kilikuwa chini ya ulinzi wa shelomothi na ndugu zake. 29 Wa uzao wa Izhari, Kenania na wana wake walikuwa wahusika wa mambo ya ndani ya Israeli. Walikuwa maafisa na waamuzi. 30 Wa uzao wa Hebroni, Hashabia na kaka zake, wanaume wenye uwezo 1, 700, walikuwa wahusika wa kazi ya Yahweh na kazi ya mfalme. Walikuwa upande wa mgharibi mwa Yordani. 31 Kutoka uzao wa Hebroni, Yeriya alikuwa kiongozi wa uzao wake, walihesabiwa kutoka orodha za familia zao. Katika mwaka wa arobaini wa utawala wa Daudi walitathimini kumbukumbu na kugundua miongoni mwao wanaume wa uwezo katika Yazeri ya Gileadi. 32 Yerija alikuwa na ndugu 2, 700, walio kuwa viongozi wenye uwezo katika familia. Daudi aliwafanya waangalizi wa makabila ya Rubeni na Gadi, na nusu kabila la Manase, kwa kila jambo linalo muhusu Mungu, na kwa mambo ya mfalme.
<- 1 Mambo ya Nyakati 251 Mambo ya Nyakati 27 ->
1 Mambo ya Nyakati