1 “Angalieni, nitamtuma mjumbe wangu, atakayeiandaa njia mbele yangu. Ndipo ghafula Bwana mnayemtafuta atakuja hekaluni mwake. Mjumbe wa agano, ambaye mnamwonea shauku, atakuja,” asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni.
2 Lakini ni nani atakayeweza kustahimili hiyo siku ya kuja kwake? Ni nani awezaye kusimama atakapotokea? Kwa kuwa atakuwa kama moto wa mfua fedha au kama sabuni ya mfua nguo. 3 Ataketi kama mfuaji na asafishaye fedha. Atawatakasa Walawi, naye atawasafisha kama dhahabu na fedha. Kisha Mwenyezi Mungu atakuwa na watu watakaoleta sadaka katika haki, 4 nazo sadaka za Yuda na Yerusalemu zitakubalika kwa Mwenyezi Mungu, kama katika siku zilizopita, kama katika miaka ya zamani.
5 “Basi nitakuja karibu nanyi ili kuhukumu. Nami nitakuwa mwepesi kushuhudia dhidi ya wachawi, wazinzi, waapao kwa uongo, wanaopunja vibarua malipo yao, wanaowadhulumu wajane na yatima, na wanaowanyima wageni haki, lakini hawaniogopi mimi,” asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni.
8 “Je, mwanadamu atamwibia Mungu? Hata hivyo mnaniibia mimi.
14 “Mmesema, ‘Ni bure kumtumikia Mungu. Tumepata faida gani kwa kushika maagizo yake na kwenda kama waombolezaji mbele za Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni? 15 Lakini sasa wenye kiburi wanabarikiwa. Hakika watenda maovu wanastawi, pia hata wale wanaoshindana na Mungu ndio wanaosalimika.’ ”
16 Ndipo wale waliomcha Mwenyezi Mungu wakasemezana wao kwa wao, naye Mwenyezi Mungu akasikiliza na akasikia. Kitabu cha kumbukumbu kikaandikwa mbele yake kuhusu wale ambao walimcha Mwenyezi Mungu na kuliheshimu jina lake.
17 “Nao watakuwa watu wangu,” asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, “katika siku ile nitakapowafanya kuwa hazina yangu ya pekee. Nitawahurumia, kama vile kwa huruma mtu amhurumiavyo mwanawe anayemtumikia. 18 Kwa mara nyingine tena utaona tofauti kati ya wenye haki na waovu, kati ya wale wanaomtumikia Mungu na wale wasiomtumikia.
<- Malaki 2Malaki 4 ->
Languages