1 Baada ya Isa kumaliza kusema haya yote kwa watu waliokuwa wanamsikiliza, akaingia Kapernaumu. 2 Mtumishi wa jemadari mmoja Mrumi, ambaye bwana wake alimthamini sana, alikuwa mgonjwa sana karibu na kufa. 3 Jemadari huyo aliposikia habari za Isa, aliwatuma wazee wa Wayahudi kwake, wakamwomba aje kumponya mtumishi wa huyo jemadari. 4 Wale wazee walipofika kwa Isa, wakamsihi sana amsaidie yule jemadari wakisema, “Mtu huyu anastahili wewe umfanyie jambo hili, 5 kwa sababu analipenda taifa letu tena ametujengea sinagogi.” 6 Hivyo Isa akaongozana nao.
9 Isa aliposikia maneno haya, alishangazwa naye sana. Akageukia umati ule wa watu waliokuwa wanamfuata, akawaambia, “Sijaona imani kubwa namna hii hata katika Israeli.” 10 Nao wale watu waliokuwa wametumwa kwa Isa waliporudi nyumbani walimkuta yule mtumishi amepona.
14 Kisha akalikaribia jeneza, akaligusa. Nao wale waliokuwa wamelibeba wakasimama. Akasema, “Kijana, nakuambia, inuka.” 15 Yule aliyekuwa amekufa akaketi akaanza kuongea, naye Isa akamkabidhi kwa mama yake.
16 Watu wote wakajawa na hofu ya Mungu, nao wakamtukuza Mungu wakisema, “Nabii mkuu ametokea miongoni mwetu. Mungu amekuja kuwakomboa watu wake.” 17 Habari hizi za mambo aliyoyafanya Isa zikaenea Yudea yote na sehemu zote za jirani.
18 Wanafunzi wa Yahya wakamweleza Yahya mambo haya yote. Hivyo Yahya akawaita wanafunzi wake wawili 19 na kuwatuma kwa Bwana Isa ili kumuuliza, “Wewe ndiwe yule aliyekuwa aje, au tumngojee mwingine?”
20 Wale watu walipofika kwa Isa wakamwambia, “Yahya ametutuma tukuulize, ‘Wewe ndiwe yule aliyekuwa aje, au tumtazamie mwingine?’ ”
21 Wakati huo huo, Isa aliwaponya wengi waliokuwa na magonjwa, maradhi na pepo wachafu, na pia akawafungua vipofu wengi macho wakapata kuona. 22 Hivyo akawajibu wale wajumbe, “Rudini mkamwambie Yahya yote mnayoyaona na kuyasikia: Vipofu wanapata kuona, viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakaswa, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa na maskini wanahubiriwa Habari Njema. 23 Amebarikiwa mtu yule asiyechukizwa na mimi.”
24 Wajumbe wa Yahya walipoondoka, Isa akaanza kusema na umati wa watu kuhusu Yahya. Akawauliza, “Mlipoenda kule nyikani, mlienda kuona nini? Je, ni unyasi ukipeperushwa na upepo? 25 Kama sivyo, mlienda kuona nini basi? Mtu aliyevaa mavazi ya kifahari? La hasha! Watu wanaovaa mavazi ya kifahari na kuishi maisha ya anasa wako katika majumba ya kifalme. 26 Lakini mlienda kuona nini? Mlienda kumwona nabii? Naam, nawaambia, yeye ni zaidi ya nabii. 27 Huyu ndiye ambaye habari zake zimeandikwa:
29 (Watu wote, hata watoza ushuru, waliposikia maneno ya Isa, walikubali kwamba mpango wa Mungu ni haki, maana walikuwa wamebatizwa na Yahya. 30 Lakini Mafarisayo[b] na wataalamu wa Torati walikataa mpango wa Mungu kwao kwa kutokubali kubatizwa na Yahya.)
31 Isa akawauliza, “Niwafananishe na nini watu wa kizazi hiki? Wanafanana na nini? 32 Wao ni kama watoto waliokaa sokoni wakiitana wao kwa wao, wakisema:
36 Basi Farisayo mmoja alimwalika Isa kwake ale chakula. Hivyo Isa akaenda nyumbani mwa yule Farisayo na kuketi mezani. 37 Palikuwa na mwanamke mmoja katika mji ule aliyekuwa mwenye dhambi. Alipopata habari kwamba Isa alikuwa akila chakula nyumbani mwa yule Farisayo, akaleta chupa ya marhamu yenye manukato. 38 Yule mwanamke akasimama nyuma ya miguu ya Isa akilia. Akailowanisha miguu yake kwa machozi yake, kisha akaifuta kwa nywele zake, akaibusu na kuimiminia manukato.
39 Yule Farisayo aliyemwalika Isa alipoona yanayotendeka, akawaza moyoni mwake, “Kama huyu mtu angekuwa nabii, angejua kwamba ni nani anayemgusa, na kwamba yeye ni mwanamke wa namna gani, na ya kuwa huyu mwanamke ni mwenye dhambi.”
40 Isa akamjibu, “Simoni, nina jambo la kukuambia.”
41 “Palikuwa na mtu mmoja aliyewakopesha watu wawili fedha: Mmoja alidaiwa dinari mia tano[c] na mwingine dinari hamsini. 42 Wote wawili walipokuwa hawawezi kulipa, aliyafuta madeni yao wote wawili. Sasa ni yupi kati yao atakayempenda zaidi yule aliyewasamehe?”
43 Simoni akajibu, “Nadhani ni yule aliyesamehewa deni kubwa zaidi.”
44 Kisha akamgeukia yule mwanamke, akamwambia Simoni, “Je, unamwona mwanamke huyu? Nilipoingia nyumbani mwako, hukunipa maji ya kunawa miguu yangu, lakini huyu ameninawisha miguu kwa machozi yake, na kunifuta kwa nywele zake. 45 Hukunisalimu kwa busu, lakini huyu mwanamke hajaacha kuibusu miguu yangu tangu nilipoingia. 46 Hukunipaka mafuta kichwani mwangu, lakini yeye ameipaka miguu yangu manukato. 47 Kwa hiyo, nakuambia, dhambi zake zilizokuwa nyingi zimesamehewa, kwani ameonesha upendo mwingi. Lakini yule aliyesamehewa kidogo, hupenda kidogo.”
48 Kisha akamwambia yule mwanamke, “Dhambi zako zimesamehewa.”
49 Lakini wale waliokuwa wameketi pamoja naye chakulani wakaanza kusemezana wao kwa wao, “Huyu ni nani ambaye hata anasamehe dhambi?”
50 Isa akamwambia yule mwanamke, “Imani yako imekuokoa; nenda kwa amani.”
<- Luka 6Luka 8 ->- a Wale ambao hawakumfahamu Isa kuwa Masihi walimwita “Bwana” kwa heshima ya kawaida.
- b Kundi la kidini la Wayahudi; walifuata Torati kwa dhati, hasa maagizo kuhusu utakaso. Pia waliamini katika malaika, ufufuo wa wafu, na kuja kwa Masihi ambaye atarejesha ufalme wa Daudi na ukuu wa taifa la Israeli.
- c Dinari 500 ni sawa na mshahara wa kibarua wa siku mia tano.
Languages