2 “ ‘Au mtu akitambua kuwa ana hatia, kama vile akigusa kitu chochote ambacho ni najisi, iwe ni mizoga ya wanyama pori walio najisi, au ya wanyama wafugwao walio najisi, au ya viumbe vinavyotambaa ardhini, hata akiwa hana habari, amekuwa najisi na mwenye hatia.
3 “ ‘Au akigusa kitu kilicho kichafu kinachotokana na binadamu, kitu chochote kile kinachoweza kumfanya awe najisi, hata akiwa hana habari, atakapofahamu atakuwa na hatia.
4 “ ‘Au kama mtu ameapa kufanya kitu chochote bila kufikiri, kiwe chema au kibaya, kwa vyovyote mtu aweza kuapa bila kujali, hata akiwa hana habari, atakapofahamu atakuwa na hatia.
5 “ ‘Mtu yeyote atakapokuwa na hatia katika mojawapo ya haya, ni lazima akiri ni kwa njia gani ametenda dhambi, 6 na kama adhabu ya dhambi aliyoitenda, ni lazima alete kwa Mwenyezi Mungu kondoo jike au mbuzi jike kutoka kundi lake kuwa sadaka ya dhambi; naye kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake kwa dhambi yake.
7 “ ‘Lakini kama huyo mtu hataweza kumtoa mwana-kondoo, ataleta hua wawili au makinda wawili wa njiwa kwa Mwenyezi Mungu ikiwa ni adhabu kwa ajili ya dhambi yake: mmoja wa hao ndege kwa ajili ya sadaka ya dhambi, na wa pili kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa. 8 Atawaleta kwa kuhani, ambaye atamtoa kwanza ndege mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi. Atamvunja shingo na kuacha kichwa chake kikining’inia, 9 naye atanyunyiza sehemu ya hiyo damu ya sadaka ya dhambi kwenye pembe za madhabahu. Damu iliyobaki lazima ichuruzwe chini ya madhabahu. Hii ni sadaka ya dhambi. 10 Kisha kuhani atamtoa yule ndege wa pili kama sadaka ya kuteketezwa kwa kufuata utaratibu uliowekwa, na hivyo kufanya upatanisho kwa ajili yake kwa dhambi aliyoitenda, naye atasamehewa.
11 “ ‘Ikiwa basi hawezi kupata hua wawili au makinda wawili wa njiwa, ataleta sehemu ya kumi ya efa[a] ya unga laini kwa ajili ya sadaka ya dhambi. Kamwe asiweke mafuta wala uvumba juu yake, kwa sababu ni sadaka ya dhambi. 12 Atauleta unga kwa kuhani, ambaye atachukua konzi moja kama sehemu ya kumbukumbu na atauteketeza kwenye madhabahu juu ya sadaka zilizotolewa kwa Mwenyezi Mungu kwa moto. Hii ni sadaka ya dhambi. 13 Kwa njia hii kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake kwa dhambi yoyote ya hizo alizotenda, naye atasamehewa. Sadaka iliyobaki itakuwa ya kuhani, kama ilivyokuwa ile sadaka ya nafaka.’ ”
17 “Kama mtu akifanya dhambi, na kutenda yaliyokatazwa katika mojawapo ya amri za Mwenyezi Mungu, hata ikiwa hajui, yeye ana hatia na anastahili adhabu. 18 Atamletea kuhani kama sadaka ya hatia kondoo dume kutoka kundi lake, kondoo asiye na dosari na mwenye thamani halisi. Kwa njia hii, kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake kwa kosa alilotenda bila kukusudia, naye atasamehewa. 19 Hii ni sadaka ya hatia; amekuwa na hatia kwa kufanya kosa dhidi ya Mwenyezi Mungu.”
<- Mambo Ya Walawi 4Mambo Ya Walawi 6 ->- a Sehemu ya kumi ya efa ni sawa na kilo moja.
Languages