6 “ ‘Akitoa kondoo au mbuzi kutoka kundi kuwa sadaka ya amani kwa Mwenyezi Mungu, atamtoa dume au jike asiye na dosari. 7 Akimtoa mwana-kondoo, atamleta mbele za Mwenyezi Mungu. 8 Ataweka mkono wake juu ya kichwa cha sadaka yake, naye atamchinja mbele ya Hema la Kukutania. Kisha wana wa Haruni watanyunyiza damu ya huyo mnyama pande zote za madhabahu. 9 Katika hiyo sadaka ya amani ataleta dhabihu iliyotolewa kwa Mwenyezi Mungu kwa moto: mafuta yake, mafuta yote ya mkia uliokatwa karibu na uti wa mgongo, mafuta yote yanayofunika sehemu za ndani au yale yanayounganika nazo, 10 figo mbili pamoja na mafuta yanayozifunika yaliyo karibu na kiuno, na kipande kirefu cha ini, ambayo utayaondoa pamoja na figo. 11 Kuhani ataviteketeza juu ya madhabahu viwe chakula, sadaka iliyotolewa kwa Mwenyezi Mungu kwa moto.
12 “ ‘Ikiwa sadaka yake ni mbuzi, ataileta mbele za Mwenyezi Mungu. 13 Ataweka mkono wake juu ya kichwa chake na kumchinja mbele ya Hema la Kukutania. Kisha wana wa Haruni watanyunyiza damu ya huyo mnyama pande zote za madhabahu. 14 Katika ile sadaka anayotoa, atatoa hii sadaka ya kuteketezwa kwa Mwenyezi Mungu: mafuta yote yanayofunika sehemu za ndani na yale yanayoungana nazo, 15 figo zote mbili pamoja na mafuta yaliyo juu yake karibu na kiuno, na kipande kirefu cha ini, ambayo atayaondoa pamoja na figo. 16 Kuhani ataviteketeza juu ya madhabahu viwe chakula, sadaka iliyotolewa kwa moto, harufu nzuri. Mafuta yote ya mnyama ni ya Mwenyezi Mungu.
17 “ ‘Hili ni agizo la kudumu kwa vizazi vijavyo, popote mnapoishi: Msile mafuta yoyote ya mnyama wala damu.’ ”
<- Mambo Ya Walawi 2Mambo Ya Walawi 4 ->
Languages