6 “ ‘Hata hivyo, nitauletea afya na uponyaji, nitawaponya watu wangu na kuwafanya wafurahie amani tele na salama. 7 Nitawarudisha Yuda na Israeli kutoka uhamishoni, na kuwajenga tena kama walivyokuwa hapo awali. 8 Nitawatakasa dhambi zote walizofanya dhidi yangu, na nitawasamehe dhambi zote za uasi dhidi yangu. 9 Kisha mji huu utaniletea utukufu, furaha, sifa na heshima mbele ya mataifa yote ya dunia yatakayosikia mambo yote mazuri ninayoufanyia. Nao watashangaa na kutetemeka kwa ajili ya wingi wa mafanikio na amani nitakayoupatia.’
10 “Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: ‘Mnasema kuhusu mahali hapa kwamba, “Ni mahali palipoachwa ukiwa, pasipo na wanadamu wala wanyama.” Lakini katika miji ya Yuda na barabara za Yerusalemu ambazo zimeachwa, ambazo hazikaliwi na wanadamu wala wanyama, huko kutasikika kwa mara nyingine 11 sauti za shangwe na furaha, sauti za bibi arusi na bwana arusi, na sauti za wale waletao sadaka za shukrani katika nyumba ya Mwenyezi Mungu, wakisema,
12 “Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni: ‘Mahali hapa, palipo ukiwa, bila wanadamu wala wanyama: katika miji yake, yatakuwa tena malisho ya wachungaji kuyalaza makundi yao. 13 Katika miji ya nchi ya vilima, ya vilima vya magharibi na ya Negebu, katika nchi ya Benyamini, katika vijiji vinavyoizunguka Yerusalemu na katika miji ya Yuda, makundi ya kondoo yatapita tena chini ya mkono wa yeye anayehesabu,’ asema Mwenyezi Mungu.
14 “ ‘Siku zinakuja,’ asema Mwenyezi Mungu, ‘wakati nitakapotimiza ahadi yangu ya rehema niliyoifanya kwa nyumba ya Israeli na kwa nyumba ya Yuda.
19 Neno la Mwenyezi Mungu likamjia Yeremia kusema: 20 “Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: ‘Ikiwa mtaweza kuvunja agano langu kuhusu usiku na mchana, ili usiku na mchana visiwepo kwa nyakati zake, 21 basi agano langu na Daudi mtumishi wangu, na agano langu na Walawi ambao ni makuhani wanaohudumu mbele zangu, linaweza kuvunjwa, na Daudi hatakuwa tena na mzao wa kutawala kwenye kiti chake cha utawala. 22 Nitawafanya wazao wa Daudi mtumishi wangu na Walawi wanaohudumu mbele zangu wengi, wasioweza kuhesabika kama nyota za angani, tena wasiopimika kama mchanga wa ufuoni mwa bahari.’ ”
23 Neno la Mwenyezi Mungu likamjia Yeremia kusema: 24 “Je, hujasikia kwamba watu hawa wanasema, ‘Mwenyezi Mungu amezikataa zile falme mbili alizozichagua’? Kwa hiyo wamewadharau watu wangu, na hawawaoni tena kama taifa. 25 Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: ‘Kama sijathibitisha agano langu na usiku na mchana, na kuziweka wakfu sheria za mbingu na nchi, 26 basi nitawakataa wazao wa Yakobo na Daudi mtumishi wangu, na sitachagua mmoja wa wanawe kutawala wazao wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo. Kwa maana nitawarudisha kutoka nchi ya kutekwa kwao na kuwaonea huruma.’ ”
<- Yeremia 32Yeremia 34 ->
Languages