Yeremia
1 Maneno ya Yeremia mwana wa Hilkia, mmoja wa makuhani katika mji wa Anathothi, katika nchi ya Benyamini. 2 Neno la Mwenyezi Mungu lilimjia katika mwaka wa kumi na tatu wa utawala wa Yosia mwana wa Amoni mfalme wa Yuda, 3 na pia wakati wa utawala wa Yehoyakimu mwana wa Yosia mfalme wa Yuda, hadi mwezi wa tano wa mwaka wa kumi na moja wa utawala wa Sedekia mwana wa Yosia mfalme wa Yuda, wakati watu wa Yerusalemu walipopelekwa uhamishoni.
6 Nami nikasema, “Aa, Bwana Mungu Mwenyezi, sijui kusema, kwani mimi ni mtoto mdogo tu.”
7 Lakini Mwenyezi Mungu akaniambia, “Usiseme, ‘Mimi ni mtoto mdogo tu.’ Utaenda popote nitakapokutuma na kunena lolote nitakalokuagiza. 8 Usiwaogope, kwa maana niko pamoja nawe nikuokoe,” asema Mwenyezi Mungu.
9 Kisha Mwenyezi Mungu akaunyoosha mkono wake na kugusa kinywa changu, akaniambia, “Sasa nimeyaweka maneno yangu kinywani mwako. 10 Tazama, leo nimekuweka juu ya mataifa na falme ili kung’oa na kubomoa, kuharibu na kuangamiza, kujenga na kupanda.”
11 Neno la Mwenyezi Mungu likanijia kusema, “Je, Yeremia unaona nini?”
12 Mwenyezi Mungu akaniambia, “Umeona vyema kwa maana ninaliangalia neno langu ili kuona kwamba limetimizwa.”
13 Neno la Mwenyezi Mungu likanijia tena, “Unaona nini?”
14 Mwenyezi Mungu akaniambia, “Kutoka kaskazini maafa yatamwagwa kwa wote wanaoishi katika nchi. 15 Nitawaita watu wote wa falme za kaskazini,” asema Mwenyezi Mungu.
17 “Jiandae! Simama useme chochote nitakachokuamuru. Usiwaogope, la sivyo nitakufanya uwaogope wao. 18 Leo nimekufanya mji wenye ngome, nguzo ya chuma, na ukuta wa shaba ili kusimama dhidi ya nchi yote: dhidi ya wafalme wa Yuda, maafisa wake, makuhani wake na watu wa nchi hiyo. 19 Watapigana nawe lakini hawatakushinda, kwa kuwa niko pamoja nawe, nami nitakuokoa,” asema Mwenyezi Mungu.
Yeremia 2 ->
Languages