5 Waisraeli wakaishi miongoni mwa Wakanaani, Wahiti, Waamori, Waperizi, Wahivi na Wayebusi. 6 Wakaoa binti za hao mataifa, na wakawatoa binti zao wenyewe waolewe na wana wa hao mataifa, na wakaitumikia miungu yao.
15 Waisraeli wakamlilia tena Mwenyezi Mungu, naye akawapa mkombozi: Ehudi, mtu wa shoto, mwana wa Gera Mbenyamini. Waisraeli wakatuma kwa Egloni mfalme wa Moabu ushuru kwa mkono wa Ehudi. 16 Basi Ehudi alikuwa ametengeneza upanga ukatao kuwili, ukiwa na urefu wa kama dhiraa moja[b], naye akaufunga upanga huo ndani ya nguo yake, kwenye paja lake la mkono wa kuume. 17 Akamkabidhi ushuru Egloni mfalme wa Moabu, aliyekuwa mtu mnene sana. 18 Baada ya Ehudi kumkabidhi ule ushuru, akawatuma wale watu waliokuwa wameubeba huo ushuru waende zao. 19 Ehudi akafuatana nao hadi kwenye sanamu za mawe karibu na Gilgali, ndipo yeye akarudi, akafika kwa Egloni na kusema, “Ee Mfalme, ninao ujumbe wa siri kwako.”
20 Ndipo Ehudi akamsogelea alipokuwa ameketi peke yake kwenye chumba cha juu cha jumba lake la kifalme la majira ya kiangazi, na kusema, “Ninao ujumbe kutoka kwa Mungu kwa ajili yako.” Mfalme alipokuwa anainuka kutoka kiti chake, 21 Ehudi akaunyoosha mkono wake wa kushoto na kuufuta ule upanga aliokuwa ameufunga kwenye paja lake la kulia, akamdunga Mfalme Egloni tumboni mwake. 22 Hata mpini nao ukazama tumboni pamoja na upanga wenyewe, nao upanga ukatokea mgongoni mwake. Ehudi hakuuchomoa huo upanga, nayo mafuta yakashikamana juu ya upanga. 23 Ehudi akatoka nje barazani; akamfungia milango ya chumba cha juu, na kuifunga kwa funguo.
24 Baada yake kuondoka, watumishi wakaja na kupata milango ya chumba cha juu imefungwa kwa funguo. Wakasema, “Bila shaka anajisaidia chumba cha ndani.” 25 Wakangoja hadi wakawa na fadhaa, na wakati hakuifungua milango ya chumba, wakachukua funguo na kuifungua. Tazama, wakaona bwana wao amelala sakafuni, amekufa.
26 Walipokuwa wangali wanangoja, Ehudi akatoroka, akapita hapo kwenye sanamu ya kuchora kwenye mawe na kukimbilia Seira. 27 Alipofika huko, akapiga tarumbeta katika nchi ya vilima ya Efraimu, nao Waisraeli wakateremka pamoja naye kutoka vilimani, yeye akiwa anawaongoza.
28 Akawaagiza, “Nifuateni, kwa kuwa Mwenyezi Mungu amewatia Moabu, adui zenu, mikononi mwenu.” Kwa hiyo wakateremka wakamfuata, wakavishika vivuko vya Yordani kuelekea Moabu, wala hawakumwacha mtu yeyote kuvuka. 29 Wakati huo wakawaua Wamoabu wapatao elfu kumi wenye nguvu na mashujaa; hakuna yeyote aliyetoroka. 30 Siku ile Moabu wakashindwa na Israeli, nayo nchi ikawa na amani kwa miaka themanini.
Languages