mkono wa Mwenyezi Mungu utajulikana kwa watumishi wake,
bali ghadhabu yake kali
itaoneshwa kwa adui zake.
15 Tazama, Mwenyezi Mungu anakuja na moto,
magari yake ya vita ni kama upepo wa kisulisuli,
atateremsha hasira yake kwa ghadhabu kali,
na karipio lake pamoja na miali ya moto.
16 Kwa maana kwa moto na kwa upanga wake
Mwenyezi Mungu atatekeleza hukumu juu ya watu wote,
nao wengi watakuwa ni wale waliouawa na Mwenyezi Mungu.
17 “Watu wote wanaojiweka wakfu na kujitakasa wenyewe ili kwenda bustanini, wakimfuata aliye katikati ya wale wanaokula nyama za nguruwe na panya pamoja na vitu vingine vilivyo machukizo, watafikia mwisho wao pamoja,” asema Mwenyezi Mungu.
18 “Nami, kwa sababu ya matendo yao na mawazo yao, niko karibu kuja na kukusanya mataifa yote na lugha zote, nao watakuja na kuuona utukufu wangu.
19 “Nitaweka ishara kati yao, nami nitapeleka baadhi ya hao walionusurika kwa mataifa, hadi Tarshishi, kwa Puli na Waludi (wanaojulikana kama wapiga upinde), kwa Tubali na Uyunani, hadi visiwa vya mbali ambavyo havijasikia kuhusu sifa zangu au kuuona utukufu wangu. Watatangaza utukufu wangu miongoni mwa mataifa. 20 Nao watawaleta ndugu zenu wote, kutoka mataifa yote, hadi mlima wangu mtakatifu huko Yerusalemu kama sadaka kwa Mwenyezi Mungu, juu ya farasi, katika magari ya vita na magari makubwa, juu ya nyumbu na ngamia,” asema Mwenyezi Mungu. “Watawaleta, kama Waisraeli waletavyo sadaka zao za nafaka, katika Hekalu la Mwenyezi Mungu, katika vyombo vilivyotakaswa. 21 Nami nitachagua baadhi yao pia wawe makuhani na Walawi,” asema Mwenyezi Mungu.
22 “Kama vile mbingu mpya na nchi mpya ninazozifanya zitakavyodumu mbele zangu,” asema Mwenyezi Mungu, “ndivyo jina lenu na wazao wenu watakavyodumu. 23 Kutoka Mwezi Mpya hata mwingine, na kutoka Sabato hadi nyingine, wanadamu wote watakuja na kusujudu mbele zangu,” asema Mwenyezi Mungu. 24 “Nao watatoka nje na kuona maiti za wale walioniasi mimi. Funza wao hawatakufa, wala moto wao hautazimika, nao watakuwa kitu cha kuchukiza sana kwa wanadamu wote.”