6 “Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni: ‘Baada ya muda kidogo kwa mara nyingine nitazitikisa mbingu na nchi, bahari na nchi kavu. 7 Nitatikisa mataifa yote, nacho kile kinachotamaniwa na mataifa yote kitakuja, nami nitaujaza utukufu katika nyumba hii,’ asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni. 8 ‘Fedha ni mali yangu na dhahabu ni mali yangu,’ asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni. 9 ‘Utukufu wa nyumba hii ya sasa utakuwa mkubwa kuliko utukufu wa ile nyumba ya mwanzoni,’ asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni. ‘Na mahali hapa nitawapa amani,’ asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni.”
13 Kisha Hagai akasema, “Je, kama mtu aliyetiwa unajisi kwa kugusa maiti akigusa mojawapo ya vitu hivi, kitu hicho kitakuwa kimetiwa unajisi?”
14 Kisha Hagai akasema, “ ‘Basi ndivyo walivyo machoni pangu hawa watu na taifa hili,’ asema Mwenyezi Mungu. ‘Lolote wafanyalo na chochote watoacho hapo ni najisi.
15 “ ‘Sasa fikirini kwa uangalifu kuanzia leo na kuendelea: tafakarini jinsi mambo yalivyokuwa kabla halijawekwa jiwe moja juu ya lingine katika Hekalu la Mwenyezi Mungu. 16 Mtu alipoendea lundo la nafaka la vipimo ishirini, kulikuwa na vipimo kumi tu. Mtu alipoendea pipa la mvinyo ili kuchota vipimo hamsini, kulikuwa na vipimo ishirini tu. 17 Kazi zenu zote za mikono nilizipiga kwa ukame, ukungu na mvua ya mawe, lakini hata hivyo, hamkunigeukia mimi,’ asema Mwenyezi Mungu. 18 ‘Tangu leo na kuendelea, kuanzia siku hii ya ishirini na nne ya mwezi wa tisa, tafakarini siku ambayo msingi wa Hekalu la Mwenyezi Mungu uliwekwa. Tafakarini: 19 Je, bado kuna mbegu iliyobakia ghalani? Hadi sasa, hakuna mzabibu au mtini, mkomamanga wala mzeituni uliozaa tunda.
23 “ ‘Katika siku ile,’ asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, ‘nitakuchukua wewe, mtumishi wangu Zerubabeli mwana wa Shealtieli,’ asema Mwenyezi Mungu. ‘Nitakufanya kama pete yangu ya muhuri, kwa kuwa nimekuchagua,’ asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni.”
<- Hagai 1
Languages