5 Ibrahimu akamwachia Isaka kila kitu alichokuwa nacho. 6 Lakini Ibrahimu alipokuwa bado hai, akawapa watoto wa masuria wake zawadi, kisha akawaondoa waende kuishi pande za mashariki mbali na mwanawe Isaka.
7 Kwa jumla, Ibrahimu aliishi miaka mia moja na sabini na tano (175). 8 Ndipo Ibrahimu akapumua pumzi ya mwisho na akafa akiwa mwenye umri mzuri, mzee aliyeshiba siku; naye akakusanywa pamoja na watu wake. 9 Watoto wake Isaka na Ishmaeli wakamzika katika pango la Makpela karibu na Mamre, katika shamba lililokuwa la Efroni mwana wa Sohari Mhiti, 10 shamba ambalo Ibrahimu alilinunua kwa Wahiti. Hapo ndipo Ibrahimu alipozikwa pamoja na mkewe Sara. 11 Baada ya kifo cha Ibrahimu, Mungu akambariki mwanawe Isaka, ambaye baadaye aliishi karibu na Beer-Lahai-Roi.
21 Isaka akamwomba Mwenyezi Mungu kwa ajili ya mke wake, kwa sababu alikuwa tasa. Mwenyezi Mungu akajibu maombi yake na Rebeka mkewe akapata mimba. 22 Watoto wakashindana tumboni mwake, naye akasema, “Kwa nini haya yanatokea kwangu?” Kwa hiyo akaenda kumuuliza Mwenyezi Mungu.
23 Mwenyezi Mungu akamjibu,
24 Wakati wake wa kujifungua ulipotimia, walikuwepo mapacha wa kiume tumboni mwake. 25 Wa kwanza kuzaliwa alikuwa mwekundu, na mwili wake wote ulikuwa kama mtu aliyevaa vazi lenye nywele; wakamwita jina Esau[b]. 26 Baadaye, ndugu yake akatoka, mkono wake ukiwa umemshika Esau kisigino; akaitwa jina Yakobo[c]. Isaka alikuwa na umri wa miaka sitini Rebeka alipowazaa.
27 Watoto wakakua. Esau akawa mwindaji hodari, mtu wa mbugani, naye Yakobo akawa mtu mtulivu, mwenye kukaa nyumbani. 28 Isaka, aliyekuwa anapendelea zaidi nyama za porini, alimpenda Esau, bali Rebeka alimpenda Yakobo.
29 Siku moja Yakobo alipika mchuzi wa dengu. Esau akarudi kutoka porini akiwa na njaa kali. 30 Esau akamwambia Yakobo, “Haraka, nipe huo mchuzi mwekundu! Nina njaa kali sana!” (Hii ndiyo sababu pia aliitwa Edomu[d].)
31 Yakobo akamjibu, “Niuzie kwanza haki yako ya mzaliwa wa kwanza.”
32 Esau akasema, “Tazama, mimi niko karibu kufa, itanifaa nini haki ya mzaliwa wa kwanza?”
33 Yakobo akamwambia, “Niapie kwanza.” Hivyo Esau akamwapia, akamuuzia Yakobo haki yake ya mzaliwa wa kwanza.
34 Ndipo Yakobo akampa Esau mkate na ule mchuzi wa dengu, naye akala na kunywa, kisha akainuka akaenda zake.
Languages