1 Wakati ule ule, Sauli alikuwa bado anazidisha vitisho vya kuua wanafunzi wa Bwana Isa, akamwendea kuhani mkuu, 2 naye akamwomba kuhani mkuu ampe barua za kwenda kwenye masinagogi huko Dameski, ili akimkuta mfuasi yeyote wa Njia Ile[a], akiwa mwanaume au mwanamke, aweze kuwafunga na kuwaleta Yerusalemu. 3 Basi akiwa katika safari yake, alipokaribia Dameski, ghafula nuru kutoka mbinguni ikamwangaza pande zote. 4 Akaanguka chini, akasikia sauti ikimwambia, “Sauli, Sauli, mbona unanitesa?”
5 Sauli akajibu, “U nani wewe, Bwana?”
7 Watu waliokuwa wakisafiri pamoja na Sauli wakasimama bila la kusema, kwa sababu walisikia sauti lakini hawakumwona aliyekuwa akizungumza. 8 Sauli akainuka kutoka pale chini na alipojaribu kufungua macho yake hakuweza kuona kitu chochote. Basi wakamshika mkono wakamwongoza hadi Dameski. 9 Kwa muda wa siku tatu alikuwa kipofu; naye hakula wala kunywa chochote.
10 Huko Dameski kulikuwa na mwanafunzi mmoja jina lake Anania. Bwana Isa alimwita katika maono, “Anania!”
11 Bwana Isa akamwambia, “Ondoka uende katika barabara iitwayo Nyofu ukaulize katika nyumba ya Yuda mtu kutoka Tarso, jina lake Sauli, kwa maana wakati huu anaomba, 12 katika maono amemwona mtu aitwaye Anania akija na kuweka mikono juu yake ili apate kuona tena.”
13 Anania akajibu, “Bwana, nimesikia kutoka kwa watu wengi habari nyingi kuhusu mtu huyu na madhara yote aliyowatendea watakatifu wako huko Yerusalemu. 14 Naye amekuja hapa Dameski akiwa na mamlaka kutoka kwa viongozi wa makuhani ili awakamate wote wanaotaja jina lako.”
15 Lakini Bwana Isa akamwambia Anania, “Nenda! Mtu huyu ni chombo nilichochagua kutangaza jina langu kwa watu wa Mataifa na wafalme wao na watu wa Israeli. 16 Nami nitamwonesha jinsi impasavyo kuteseka kwa ajili ya Jina langu.”
17 Kisha Anania akaenda kwenye ile nyumba, akaingia ndani. Akaweka mikono yake juu ya Sauli akasema, “Ndugu Sauli, Bwana Isa aliyekutokea njiani amenituma kwako ili upate kuona tena na ujazwe Roho Mtakatifu wa Mungu.” 18 Ghafula vitu kama magamba vikaanguka chini, kutoka machoni mwa Sauli, akapata kuona tena. Akasimama, akabatizwa. 19 Baada ya kula chakula, akapata nguvu tena. Sauli akakaa siku kadhaa pamoja na wanafunzi huko Dameski.
23 Baada ya siku nyingi kupita, Wayahudi wakapanga njama kumuua Sauli. 24 Lakini Sauli akagundua njama yao. Wayahudi wakawa wanalinda malango yote ya mji, usiku na mchana ili wapate kumuua. 25 Lakini wafuasi wake wakamchukua usiku wakamshusha akiwa ndani ya kapu kupitia mahali penye nafasi ukutani.
31 Ndipo waumini katika Yudea yote, Galilaya na Samaria wakawa na wakati wa amani. Likatiwa nguvu; na kwa kuwezeshwa na Roho wa Mungu, idadi yao ikaongezeka, na wakaendelea kudumu katika kumcha Bwana.
39 Kwa hiyo Petro akainuka akaenda nao. Alipowasili, wakampeleka hadi kwenye chumba cha ghorofani alipokuwa amelazwa. Wajane wengi walisimama karibu naye wakilia na kuonesha majoho na nguo nyingine ambazo Dorkasi alikuwa amewashonea alipokuwa pamoja nao.
40 Petro akawatoa wote nje ya kile chumba, kisha akapiga magoti akaomba, akaugeukia ule mwili akasema, “Tabitha, inuka.” Akafumbua macho yake na alipomwona Petro, akaketi. 41 Petro akamshika mkono akamwinua, ndipo akawaita wale watakatifu na wajane akamkabidhi kwao akiwa hai. 42 Habari hizi zikajulikana sehemu zote za Yafa na watu wengi wakamwamini Bwana Isa. 43 Petro akakaa Yafa kwa siku nyingi akiishi na Simoni mtengenezaji ngozi.
<- Matendo Ya Mitume 8Matendo Ya Mitume 10 ->- a Njia Ile maana yake wafuasi wa Isa (Yohana 14:6; Matendo 24:14); walichukuliwa kuwa dhehebu la dini ya Wayahudi.
- b Yaani Mwana wa asili moja na Mwenyezi Mungu (Yohana 1:1-2), wa kiroho, bali si wa kimwili.
- c Al-Masihi maana yake Aliyetiwa mafuta.
- d Tabitha kwa Kiaramu na Dorkasi kwa Kiyunani yote yamaanisha Paa.
Languages