5 Lakini Wayahudi ambao hawakuwa wameamini wakawa na wivu, wakawakodi watu waovu kutoka sokoni, wakakutanisha umati wa watu, wakaanzisha ghasia mjini. Wakaenda mbio nyumbani mwa Yasoni wakiwatafuta Paulo na Sila ili kuwaleta nje penye umati ule wa watu. 6 Lakini walipowakosa wakamburuta Yasoni na ndugu wengine mbele ya maafisa wa mji, wakipaza sauti na kusema: “Watu hawa walioupindua ulimwengu wamekuja huku, 7 naye Yasoni amewakaribisha nyumbani mwake. Hawa wote wanaasi amri za Kaisari wakisema yuko mfalme mwingine aitwaye Isa.” 8 Waliposikia haya, umati ule wa watu na maafisa wa mji wakaongeza ghasia. 9 Nao baada ya kuchukua dhamana kwa ajili ya Yasoni na wenzake wakawaachia waende zao.
13 Lakini wale Wayahudi wa Thesalonike waliposikia kuwa Paulo anahubiri neno la Mungu huko Beroya, wakaenda huko ili kuwashawishi watu na kuwachochea. 14 Mara hiyo, wale ndugu wakamsafirisha Paulo hadi pwani, lakini Sila na Timotheo wakabaki Beroya. 15 Wale waliomsindikiza Paulo wakaenda naye hadi Athene, kisha wakarudi Beroya wakiwa na maagizo kutoka kwa Paulo kuhusu Sila na Timotheo kwamba wamfuate upesi iwezekanavyo.
22 Ndipo Paulo akasimama katikati ya mkutano wa Areopago, akasema, “Enyi watu wa Athene! Ninaona kwamba katika kila jambo ninyi ni watu wa dini sana. 23 Kwa kuwa nilipokuwa nikitembea mjini na kuangalia kwa makini vitu vyenu vya kuabudiwa, niliona huko madhabahu moja iliyoandikwa:
24 “Mungu aliyeumba dunia na vyote vilivyomo, ndiye Bwana wa mbingu na nchi; hakai katika mahekalu yaliyojengwa kwa mikono ya wanadamu. 25 Wala hatumikiwi na mikono ya wanadamu kana kwamba anahitaji chochote, kwa sababu yeye mwenyewe ndiye awapaye watu wote uhai na pumzi na vitu vyote. 26 Kutoka kwa mtu mmoja, yeye aliumba mataifa yote ya wanadamu ili waikalie dunia yote, naye akaweka nyakati za kuishi. 27 Mungu alifanya hivyo ili wanadamu wamtafute na huenda wakamfikia ingawa kwa kupapasapapasa ijapokuwa kwa kweli hakai mbali na kila mmoja wetu. 28 ‘Kwa kuwa ndani yake tunaishi, tunatembea na kuwa na uzima wetu.’ Kama baadhi ya watunga mashairi wenu walivyosema, ‘Sisi ni uzao wake.’
29 “Kwa kuwa sisi ni uzao wa Mungu, haitupasi kudhani kuwa uungu ni kama sanamu ya dhahabu au ya fedha au ya jiwe, mfano uliotengenezwa kwa ubunifu na ustadi wa mwanadamu. 30 Zamani wakati wa ujinga, Mungu alijifanya kama haoni, lakini sasa anawaamuru watu wote kila mahali watubu. 31 Kwa kuwa ameweka siku ambayo atauhukumu ulimwengu kwa haki akimtumia mtu aliyemchagua. Amewahakikishia watu wote mambo haya kwa kumfufua Al-Masihi kutoka kwa wafu.”
32 Waliposikia habari za ufufuo wa wafu, baadhi yao wakadhihaki, lakini wengine wakasema, “Tunataka kukusikia tena ukizungumza juu ya jambo hili.” 33 Kwa hiyo Paulo akaondoka katikati yao. 34 Lakini baadhi yao wakaungana naye wakaamini. Kati yao walikuwemo Dionisio, mmoja wa mkutano wa Areopago, na mwanamke mmoja aliyeitwa Damari, na wengine wengi.
<- Matendo Ya Mitume 16Matendo Ya Mitume 18 ->- a Al-Masihi maana yake Aliyetiwa mafuta.
- b Waepikureo waliamini kwamba anasa aina mbalimbali, hasa za mawazo, ndizo lengo la maisha.
- c Wastoiko waliamini kwamba maisha hayapaswi kuwa ya hisia ya furaha wala huzuni kupita kiasi.
- d maana yake baraza la viongozi au wanafalsafa wa mji wa Athene; walikutana katika kilima cha Aresi
Languages