Matendo Ya Mitume
6 Mitume walipokuwa wamekusanyika pamoja, wakamuuliza Isa, “Bwana, je, huu ndio wakati wa kuwarudishia Israeli ufalme?”
7 Isa akawaambia, “Sio wajibu wenu kujua nyakati au majira ambayo Baba ameyaweka kwa mamlaka yake mwenyewe. 8 Lakini mtapokea nguvu, Roho wa Mungu akiwajilia juu yenu, nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na Yudea yote, na Samaria, na miisho ya dunia.”
9 Baada ya kusema mambo haya, walipokuwa wanatazama, akachukuliwa juu mbinguni mbele ya macho yao na wingu likampokea wasimwone tena.
10 Walipokuwa bado wakikaza macho yao kuelekea juu alipokuwa akienda zake mbinguni, ghafula, wanaume wawili waliovaa mavazi meupe wakasimama karibu nao. 11 Wakasema, “Enyi watu wa Galilaya, mbona mnasimama mkitazama juu angani? Huyu Isa aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda mbinguni, atarudi tena jinsi hiyo hiyo mlivyomwona akienda zake mbinguni.”
12 Ndipo waliporudi Yerusalemu kutoka Mlima wa Mizeituni, uliokuwa karibu na Yerusalemu, umbali wa mwendo wa Sabato[c] kutoka mjini. 13 Walipowasili mjini Yerusalemu, walienda ghorofani kwenye chumba walichokuwa wakiishi. Waliokuwepo walikuwa:
15 Katika siku hizo Petro akasimama katikati ya waumini (jumla yao walikuwa watu wapatao mia moja na ishirini), akasema, 16 “Ndugu zangu, ilibidi andiko litimie, ambalo Roho wa Mungu alitabiri kupitia kwa Daudi kumhusu Yuda, aliyewaongoza wale waliomkamata Isa. 17 Yuda alikuwa mmoja wetu, kwa maana na yeye alichaguliwa ashiriki katika huduma hii.”
18 (Basi Yuda alinunua shamba kwa zile fedha za uovu alizopata; akiwa huko shambani akaanguka, akapasuka na matumbo yote yakatoka nje. 19 Kila mtu Yerusalemu akasikia habari hizi, kwa hiyo wakapaita mahali hapo kwa lugha yao, Akeldama, yaani Shamba la Damu.)
20 “Kama vile ilivyoandikwa katika Kitabu cha Zaburi,
23 Wakapendekeza majina ya watu wawili: Yusufu, aitwaye Barsaba (ambaye pia alijulikana kama Yusto) na Mathiya. 24 Kisha wakaomba, wakasema, “Mwenyezi Mungu, wewe waujua moyo wa kila mtu. Tuoneshe ni yupi kati ya hawa wawili uliyemchagua 25 ili achukue nafasi ya huduma ya utume, ambayo Yuda aliiacha ili aende anapostahili.” 26 Kisha wakawapigia kura, nayo kura ikamwangukia Mathiya, naye akaongezwa kwenye wale mitume kumi na mmoja.
Matendo Ya Mitume 2 ->- a Jina Baba linaonesha uhusiano maalum wa Isa na Mwenyezi Mungu.
- b Ubatizo ni ishara ya kuungama dhambi na kusamehewa na Mwenyezi Mungu, na kuweka nadhiri ya kubadilisha mienendo ya awali. Wafuasi wa Isa Al-Masihi pia wanapokea Roho wa Mungu kama dhibitisho ya imani yao.
- c kama kilomita moja
- d Wazelote walikuwa kikundi cha Kiyahudi wenye imani kali waliompinga Kaisari na utawala wa Rumi.
Languages