5 Je, hamkumbuki kwamba nilipokuwa pamoja nanyi niliwaambia mambo haya? 6 Nanyi sasa mnajua kinachomzuia, ili apate kudhihirishwa wakati wake utakapowadia. 7 Maana ile nguvu ya siri ya uasi tayari inatenda kazi, lakini yule anayeizuia ataendelea kufanya hivyo hadi atakapoondolewa. 8 Hapo ndipo yule mwasi atafunuliwa, ambaye Bwana Isa atamteketeza kwa pumzi ya kinywa chake na kumwangamiza kabisa kwa utukufu wa kuja kwake. 9 Kuja kwa yule mwasi kutalingana na vile Shetani hufanya kazi. Atatumia nguvu za aina mbalimbali katika miujiza, na ishara na ajabu za uongo, 10 na katika njia zote ambazo uovu hudanganya wanaoangamia. Wanaangamia kwa sababu walikataa kuipenda kweli ili wapate kuokolewa. 11 Kwa sababu hii, Mungu anawatumia nguvu ya udanganyifu, ili waamini uongo, 12 na hivyo wahukumiwe wote ambao hawakuiamini ile kweli, bali wamefurahia uovu.
15 Hivyo basi, ndugu wapendwa, simameni imara na myashike sana yale mafundisho tuliyowapa ikiwa ni kwa maneno ya kinywa au kwa barua.
16 Bwana wetu Isa Al-Masihi mwenyewe na Mungu, Baba yetu, aliyetupenda na kwa neema yake akatupatia faraja ya milele na tumaini jema, 17 awafariji mioyo yenu na kuwaimarisha katika kila neno na tendo jema.
<- 2 Wathesalonike 12 Wathesalonike 3 ->
Languages