2 Mfalme Daudi akamuuliza Siba, “Kwa nini umeleta vitu hivi?”
3 Kisha mfalme akauliza, “Yuko wapi mwana wa bwana wako?”
4 Ndipo mfalme akamwambia Siba, “Yote yaliyokuwa mali ya Mefiboshethi sasa ni mali yako.”
9 Ndipo Abishai mwana wa Seruya akamwambia mfalme, “Kwa nini huyu mbwa mfu amlaani bwana wangu mfalme? Niruhusu nivuke nikatilie mbali kichwa chake.”
10 Lakini mfalme akamwambia, “Mna nini nami, enyi wana wa Seruya? Ikiwa analaani kwa sababu Mwenyezi Mungu amemwambia, ‘Mlaani Daudi,’ nani awezaye kuuliza, ‘Kwa nini unafanya hivi?’ ”
11 Ndipo Daudi akamwambia Abishai na maafisa wake wote, “Mwanangu, ambaye ametoka viunoni mwangu mwenyewe, anajaribu kuniua. Je, si zaidi sana huyu Mbenyamini! Mwacheni; acha alaani, kwa maana Mwenyezi Mungu amemwambia afanye hivyo. 12 Inawezekana kwamba Mwenyezi Mungu ataona dhiki yangu na kunilipa mema kwa ajili ya laana ninayopokea leo.”
13 Kwa hiyo Daudi na watu wake wakaendelea na safari yao barabarani, huku Shimei akiwa anatembea pembezoni mwa kilima sambamba na Daudi, huku akimlaani na kumtupia Daudi mawe na kumrushia mavumbi. 14 Mfalme na watu wote aliokuwa pamoja nao wakafika kwenye kituo chao wakiwa wamechoka. Mfalme akajiburudisha hapo.
17 Absalomu akamuuliza Hushai, “Je, huu ndio upendo unaomwonesha rafiki yako? Kwa nini hukufuatana na rafiki yako?”
18 Hushai akamwambia Absalomu, “La hasha! Yeye aliyechaguliwa na Mwenyezi Mungu, aliyechaguliwa na watu hawa, atakayechaguliwa tena na wanaume wote wa Israeli, huyu ndiye nitakayekuwa wake, nami nitabakia pamoja naye. 19 Zaidi ya hayo, nimtumikie nani? Je, nisimtumikie mwana? Kama vile nilivyomtumikia baba yako, ndivyo nitakavyokutumikia wewe.”
20 Absalomu akamwambia Ahithofeli, “Tupe ushauri wako. Tufanye nini?”
21 Ahithofeli akamjibu Absalomu, “Kutana kimwili na masuria wa baba yako aliowaacha kutunza jumba la kifalme. Ndipo Israeli yote itakaposikia kwamba umejifanya chukizo kwa baba yako, nayo mikono ya kila mmoja aliye pamoja nawe itatiwa nguvu.” 22 Kwa hiyo wakamtengenezea Absalomu hema juu ya dari, naye akakutana kimwili na masuria wa baba yake machoni pa Israeli wote.
23 Ilikuwa katika siku hizo shauri lililotolewa na Ahithofeli lilikuwa kama lile ambalo limeulizwa kwa Mungu. Ndivyo Daudi na Absalomu walivyoyaheshimu mashauri yote ya Ahithofeli.
<- 2 Samweli 152 Samweli 17 ->
Languages