1 Baada ya kifo cha Sauli, Daudi alirudi kutoka kuwashinda Waamaleki, na akakaa siku mbili huko Siklagi. 2 Siku ya tatu akaja mtu mwenye nguo zilizoraruka na mavumbi kichwani mwake kutoka kambi ya Sauli. Alipomjia Daudi, akajitupa chini ili kumpa heshima.
Akasema, “Watu walikimbia kutoka vitani. Wengi wao walianguka na kufa. Naye Sauli na Yonathani mwanawe wamekufa.”
5 Ndipo Daudi akamwambia huyo kijana aliyemletea taarifa, “Je, umefahamu vipi kwamba Sauli na Yonathani mwanawe wamekufa?”
6 Yule kijana akasema, “Nilijipata huko Mlima Gilboa, naye Sauli alikuwa huko akiegemea mkuki wake, na magari ya vita na wapanda farasi wa upande wa adui wakawa wamemkaribia sana. 7 Alipogeuka na kuniona, akaniita, nami nikasema, ‘Je, nifanye nini?’
8 “Akaniuliza, ‘Wewe ni nani?’
“Nikamjibu, ‘Mimi ni Mwamaleki.’
9 “Kisha akaniambia, ‘Nikaribie mimi na uniue! Niko katika maumivu makali ya kifo, lakini bado ningali hai.’
10 “Kwa hiyo nikamkaribia na kumuua, kwa sababu nilijua kwamba baada ya kuanguka hangeweza kupona. Nami nikachukua lile taji lililokuwa kichwani mwake na utepe uliokuwa mkononi mwake, nami nimevileta hapa kwa bwana wangu.”
11 Ndipo Daudi pamoja na watu wote waliokuwa pamoja naye wakazishika nguo zao na kuzirarua. 12 Wakaomboleza, wakalia pia na kufunga hadi jioni kwa ajili ya Sauli na Yonathani mwanawe, kwa ajili ya jeshi la Mwenyezi Mungu na nyumba ya Israeli, kwa sababu wameanguka kwa upanga.
14 Daudi akamuuliza, “Kwa nini hukuogopa kuinua mkono wako ili kumwangamiza mpakwa mafuta wa Mwenyezi Mungu?”
15 Kisha Daudi akamwita mmoja wa watu wake na kumwambia, “Nenda ukamuue!” Kwa hiyo akampiga, naye akafa. 16 Kwa maana Daudi alikuwa amemwambia, “Damu yako iwe juu ya kichwa chako mwenyewe. Kinywa chako mwenyewe kimeshuhudia dhidi yako uliposema, ‘Nilimuua mpakwa mafuta wa Mwenyezi Mungu.’ ”
Ombolezo la Daudi kwa ajili ya Sauli na Yonathani
17 Daudi akafanya maombolezo haya kuhusu Sauli na Yonathani mwanawe, 18 naye akaagiza kwamba watu wa Yuda wafundishwe ombolezo hili la upinde (ambalo limeandikwa katika Kitabu cha Yashari):
19 “Walio fahari yako, ee Israeli,
wameuawa juu ya mahali pako palipoinuka.
Tazama jinsi mashujaa walivyoanguka!
20 “Msilisimulie hili katika Gathi,
msilitangaze hili katika
barabara za Ashkeloni,
binti za Wafilisti wasije wakafurahia,
binti za hao wasiotahiriwa
wasije wakashangilia.
21 “Enyi milima ya Gilboa,
msipate umande wala mvua,
wala mashamba yanayozaa sadaka ya nafaka.
Kwa maana huko ndiko ngao ya mwenye nguvu iliponajisiwa,