1 Katika mwaka wa ishirini na saba wa utawala wa Yeroboamu mfalme wa Israeli, Azaria mwana wa Amazia mfalme wa Yuda alianza kutawala. 2 Alikuwa na umri wa miaka kumi na sita alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu kwa miaka hamsini na mbili. Mama yake aliitwa Yekolia, kutoka Yerusalemu. 3 Akatenda yaliyo mema machoni pa Mwenyezi Mungu, kama Amazia baba yake alivyofanya. 4 Hata hivyo, mahali pa juu pa kuabudia hapakuondolewa. Watu waliendelea kutoa kafara na kufukiza uvumba huko.
5 Mwenyezi Mungu akampiga mfalme kwa ukoma hadi siku aliyokufa, naye aliishi katika nyumba iliyotengwa peke yake. Yothamu mwana wa mfalme akawa msimamizi wa jumba la mfalme, na akawatawala watu wa nchi.
6 Kuhusu matukio mengine ya utawala wa Azaria na yote aliyoyafanya, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Yuda? 7 Azaria akalala na baba zake, naye akazikwa karibu nao katika Mji wa Daudi. Naye Yothamu mwanawe akawa mfalme baada yake.
10 Shalumu mwana wa Yabeshi akapanga njama dhidi ya Zekaria. Akamshambulia mbele ya watu, akamuua, na akawa mfalme baada yake. 11 Matukio mengine ya utawala wa Zekaria yameandikwa kwenye kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Israeli. 12 Kwa hiyo neno la Mwenyezi Mungu lililonenwa kwa Yehu likatimia, kwamba, “Wazao wako wataketi kwenye kiti cha utawala cha Israeli hadi kizazi cha nne.”
15 Matukio mengine ya utawala wa Shalumu, na njama alizozipanga, yameandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Israeli.
16 Wakati ule, akianzia Tirsa, Menahemu alishambulia Tifsa na kila mtu ndani yake, na wale waliokuwa maeneo jirani, kwa sababu walikataa kufungua malango yao. Akaiangamiza Tifsa yote, na kuwapasua tumbo wanawake wote wenye mimba.
19 Kisha Pulu mfalme wa Ashuru akaishambulia Israeli. Menahemu mfalme wa Israeli akampa talanta elfu moja[a] za fedha ili amsaidie na kumwezesha katika utawala wake. 20 Menahemu akatoza fedha hizi kwa nguvu kutoka kwa Israeli. Kila mtu tajiri alilazimika kuchanga shekeli hamsini[b] za fedha ambazo alipewa mfalme wa Ashuru. Basi mfalme wa Ashuru akajiondoa na hakuendelea kuikalia nchi.
21 Kuhusu matukio mengine ya utawala wa Menahemu na yote aliyoyafanya, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Israeli? 22 Menahemu akalala na baba zake. Naye Pekahia mwanawe akawa mfalme baada yake.
26 Matukio mengine ya utawala wa Pekahia na yote aliyoyafanya yameandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Israeli.
29 Wakati wa utawala wa Peka mfalme wa Israeli, Tiglath-Pileseri mfalme wa Ashuru alikuja na kuteka Iyoni, Abel-Beth-Maaka, Yanoa, Kedeshi na Hazori. Akateka miji ya Gileadi na Galilaya, pamoja na nchi yote ya Naftali, na kuwahamishia watu wote Ashuru. 30 Kisha Hoshea mwana wa Ela akapanga njama dhidi ya Peka mwana wa Remalia. Hoshea akamshambulia Peka na kumuua, kisha akawa mfalme baada yake katika mwaka wa ishirini wa Yothamu mwana wa Uzia.
31 Kuhusu matukio mengine ya utawala wa Peka na yote aliyoyafanya, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Israeli?
32 Katika mwaka wa pili wa utawala wa Peka mwana wa Remalia mfalme wa Israeli, Yothamu mwana wa Uzia mfalme wa Yuda alianza kutawala. 33 Alikuwa na umri wa miaka ishirini na tano alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu miaka kumi na sita. Mama yake aliitwa Yerusha binti Sadoki. 34 Akafanya yaliyo mema machoni pa Mwenyezi Mungu, kama Uzia baba yake alivyokuwa amefanya. 35 Hata hivyo, mahali pa juu pa kuabudia hapakuondolewa. Watu waliendelea kutoa kafara na kufukiza uvumba huko. Yothamu akajenga upya Lango la Juu la Hekalu la Mwenyezi Mungu.
36 Kuhusu matukio mengine ya utawala wa Yothamu na yale aliyoyafanya, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Yuda? 37 (Katika siku hizo, Mwenyezi Mungu akaanza kuwatuma Resini mfalme wa Aramu na Peka mwana wa Remalia dhidi ya Yuda.) 38 Yothamu akalala na baba zake, akazikwa pamoja nao katika Mji wa Daudi, mji wa baba zake. Naye Ahazi mwanawe akawa mfalme baada yake.
<- 2 Wafalme 142 Wafalme 16 ->
Languages