8 Pia huko Yerusalemu, Yehoshafati akaweka baadhi ya Walawi, makuhani na viongozi wa jamaa za Waisraeli ili kutoa hukumu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kuamua magomvi. Nao waliishi huko Yerusalemu. 9 Akawapa maagizo haya: “Ni lazima mtumike kwa uaminifu na kwa moyo wote katika kicho cha Mwenyezi Mungu. 10 Katika kila shauri lifikalo mbele yenu kutoka kwa ndugu zenu wanaoishi katika miji, ikiwa ni la umwagaji wa damu au mambo mengine kuhusu sheria, amri, hukumu au maagizo, inawapasa ninyi kuwaonya kwamba wasiingie katika hatia dhidi ya Mwenyezi Mungu, la sivyo ghadhabu yake itakuja juu yenu na ndugu zenu. Tendeni hivyo, nanyi hamtatenda dhambi.
11 “Amaria kuhani mkuu atakuwa juu yenu katika jambo lolote linalomhusu Mwenyezi Mungu naye Zebadia mwana wa Ishmaeli, kiongozi wa kabila la Yuda, atakuwa juu yenu kwa jambo lolote linalomhusu mfalme, nao Walawi watatumika kama maafisa mbele yenu. Tendeni kwa ujasiri, naye Mwenyezi Mungu atakuwa pamoja na wale watendao vyema.”
<- 2 Mambo Ya Nyakati 182 Mambo Ya Nyakati 20 ->
Languages