2 Sauli alichagua watu elfu tatu kutoka Israeli; miongoni mwa hao, watu elfu mbili walikuwa naye huko Mikmashi na katika nchi ya vilima ya Betheli; nao watu elfu moja walikuwa na Yonathani huko Gibea ya Benyamini. Watu waliosalia aliwarudisha nyumbani mwao.
3 Yonathani akashambulia ngome ya Wafilisti huko Geba, nao Wafilisti wakapata habari hizo. Kisha Sauli akaamuru tarumbeta ipigwe nchi yote na kusema, “Waebrania na wasikie!” 4 Hivyo Israeli wote wakasikia habari kwamba: “Sauli ameshambulia ngome ya Wafilisti, na sasa Israeli wamekuwa harufu mbaya kwa Wafilisti.” Basi watu waliitwa kuungana na Sauli huko Gilgali.
5 Wafilisti wakakusanyika ili kupigana na Israeli, wakiwa na magari ya vita elfu tatu, waendesha magari ya vita elfu sita, na askari wa miguu wengi kama mchanga wa ufuoni mwa bahari. Walipanda na kupiga kambi huko Mikmashi, mashariki mwa Beth-Aveni. 6 Waisraeli walipoona kuwa hali yao ni ya hatari na kuwa jeshi lao limesongwa sana, wakajificha katika mapango na katika vichaka, katika miamba, kwenye mashimo na kwenye mahandaki. 7 Hata baadhi ya Waebrania wakavuka Yordani hadi nchi ya Gadi na Gileadi.
11 Samweli akamuuliza, “Umefanya nini?”
13 Samweli akamwambia Sauli, “Umetenda kwa upumbavu. Hukuyashika maagizo ya Mwenyezi Mungu, Mungu wako, aliyokupa. Kama ungetii, angeudumisha ufalme wako juu ya Israeli kwa wakati wote. 14 Lakini sasa ufalme wako hautadumu; Mwenyezi Mungu amemtafuta mtu aupendezaye moyo wake, na amemchagua awe kiongozi wa watu wake, kwa sababu hukuyatii maagizo ya Mwenyezi Mungu.”
15 Kisha Samweli akaondoka Gilgali, akapanda Gibea ya Benyamini, naye Sauli akawahesabu watu aliokuwa nao. Jumla yao walikuwa watu mia sita.
19 Hapakuwa na mhunzi ambaye angeweza kupatikana katika nchi yote ya Israeli, kwa sababu Wafilisti walikuwa wamesema, “Waebrania wasije wakatengeneza panga au mikuki!” 20 Hivyo Waisraeli wote waliteremka kwa Wafilisti ili kila mtu kunoa plau yake, jembe lake, shoka lake, au mundu wake. 21 Bei ilikuwa fedha theluthi mbili za shekeli[a] kunoa majembe ya plau na majembe ya mkono, na theluthi moja ya shekeli[b] kunoa uma, na shoka, na mchokoo.
22 Kwa hiyo siku ya vita hakuna askari yeyote kambini na Sauli na Yonathani aliyekuwa na upanga wala mkuki mkononi mwake; Sauli na mwanawe Yonathani tu ndio walikuwa navyo.
Languages