1 Hiramu mfalme wa Tiro aliposikia kuwa Sulemani amepakwa mafuta awe mfalme mahali pa Daudi baba yake, akatuma wajumbe kwa Sulemani, kwa sababu Hiramu siku zote alikuwa na uhusiano mzuri wa kirafiki na Daudi. 2 Sulemani akapeleka ujumbe huu kwa Hiramu:
7 Hiramu aliposikia ujumbe wa Sulemani, akafurahishwa sana akasema, “Ahimidiwe Mwenyezi Mungu leo, kwa kuwa amempa Daudi mwana mwenye hekima ya kutawala taifa hili kubwa.”
8 Hivyo Hiramu akapeleka ujumbe kwa Sulemani:
10 Kwa njia hii Hiramu akampa Sulemani miti yote ya mierezi na magogo ya misunobari kama alivyohitaji, 11 naye Sulemani akampa Hiramu kori elfu ishirini[a] za ngano kama chakula kwa ajili ya watu wa nyumbani mwake, pamoja na mafuta safi ya zeituni yaliyokamuliwa bathi elfu ishirini[b]. Sulemani aliendelea kumfanyia Hiramu hivyo mwaka baada ya mwaka. 12 Mwenyezi Mungu akampa Sulemani hekima, kama alivyomwahidi. Palikuwa na uhusiano wa amani kati ya Hiramu na Sulemani, na wote wawili wakafanya mkataba.
13 Mfalme Sulemani akakusanya wafanyakazi elfu thelathini kutoka Israeli yote. 14 Akawapeleka Lebanoni kwa zamu za watu elfu kumi kila mwezi. Hivyo walikaa Lebanoni kwa mwezi mmoja, na miezi miwili wakakaa nyumbani. Adoniramu ndiye alikuwa kiongozi wa shokoa. 15 Sulemani alikuwa na wachukuzi wa mizigo elfu sabini, na wachonga mawe elfu themanini huko vilimani, 16 pamoja na wasimamizi elfu tatu mia tatu ambao walisimamia mradi huo na kuwaelekeza wafanyakazi. 17 Kwa amri ya mfalme, walitoa mawe makubwa na bora kwenye machimbo ya mawe kwa kujengea msingi wa mawe yaliyochongwa kwa ajili ya Hekalu. 18 Mafundi wa Sulemani, wa Hiramu na watu wa Gebali[c] walikata na kuandaa mbao na mawe kwa ajili ya ujenzi wa Hekalu.
<- 1 Wafalme 41 Wafalme 6 ->
Languages