1 21 Ndipo neno la Mwenyezi Mungu likamjia Yehu mwana wa Hanani dhidi ya Baasha, kusema: 2 “Nilikuinua kutoka mavumbini na kukufanya mtawala wa watu wangu Israeli, lakini ukaenenda katika njia za Yeroboamu na kusababisha watu wangu Israeli kutenda dhambi na kunikasirisha kwa dhambi zao. 3 Basi nitamwangamiza Baasha pamoja na nyumba yake, nami nitaifanya nyumba yako kama ile ya Yeroboamu mwanawe Nebati. 4 Mbwa watawala walio wa nyumba ya Baasha watakaofia ndani ya mji, na ndege wa angani watawala wale watakaofia mashambani.”
5 Kuhusu matukio mengine ya utawala wa Baasha, aliyoyafanya na mafanikio yake, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Israeli? 6 Baasha akalala na baba zake naye akazikwa huko Tirsa. Naye Ela mwanawe akawa mfalme baada yake.
7 Zaidi ya hayo, neno la Mwenyezi Mungu likamjia Baasha pamoja na nyumba yake kupitia kwa nabii Yehu mwana wa Hanani, kwa sababu ya maovu yote aliyokuwa ametenda machoni pa Mwenyezi Mungu, akimkasirisha kwa mambo aliyotenda, na kuwa kama nyumba ya Yeroboamu aliyoiangamiza.
9 Zimri, mmoja wa maafisa wake, aliyekuwa na amri juu ya nusu ya magari yake ya vita, akapanga njama dhidi ya Ela. Wakati huo Ela alikuwa Tirsa, akilewa katika nyumba ya Arsa, aliyekuwa msimamizi wa jumba la kifalme huko Tirsa. 10 Zimri akaingia, akampiga na kumuua katika mwaka wa ishirini na saba wa utawala wa Asa mfalme wa Yuda. Kisha Zimri akawa mfalme baada yake.
11 Mara tu alipoanza kutawala na kukalia kiti chake cha kifalme, aliua jamaa yote ya Baasha. Hakumwacha mwanaume hata mmoja, akiwa ni ndugu au rafiki. 12 Hivyo, Zimri akawaangamiza jamaa yote ya Baasha, kama Mwenyezi Mungu alivyonena dhidi ya Baasha kupitia kwa nabii Yehu: 13 kwa sababu ya dhambi zote Baasha na mwanawe Ela walizokuwa wametenda na wakasababisha Israeli kuzitenda, basi wakamkasirisha Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, kwa sanamu zao batili.
14 Kuhusu matukio mengine ya utawala wa Ela, na yote aliyoyafanya, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Israeli?
20 Kuhusu matukio mengine ya utawala wa Zimri, na uasi alioutenda, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Israeli?
23 Katika mwaka wa thelathini na moja wa utawala wa Asa mfalme wa Yuda, Omri akawa mfalme wa Israeli, naye akatawala kwa miaka kumi na mbili, sita kati ya hiyo katika Tirsa. 24 Alinunua kilima cha Samaria kutoka kwa Shemeri kwa talanta mbili[a] za fedha na akajenga mji juu ya hicho kilima, akiuita Samaria, kutokana na Shemeri, jina la mmiliki wa kwanza wa kilima hicho.
25 Lakini Omri akatenda maovu machoni pa Mwenyezi Mungu na kutenda dhambi kuliko wote waliomtangulia. 26 Akaenenda katika njia zote za Yeroboamu mwana wa Nebati na katika dhambi zake, ambazo alisababisha Israeli kutenda, hivyo basi wakamkasirisha Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, kwa sanamu zao batili.
27 Kuhusu matukio mengine ya utawala wa Omri, yale aliyofanya na mafanikio aliyokuwa nayo, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Israeli? 28 Omri akalala na baba zake, akazikwa huko Samaria. Naye Ahabu mwanawe akawa mfalme baada yake.
34 Wakati wa Ahabu, Hieli ule Mbetheli, akaijenga Yeriko upya. Aliweka misingi yake kwa gharama ya mzaliwa wake wa kwanza Abiramu, na kuweka malango yake kwa gharama ya mwanawe mdogo Segubu, kama Mwenyezi Mungu alivyonena kupitia kwa Yoshua, mwana wa Nuni.
<- 1 Wafalme 151 Wafalme 17 ->- a Talanta 2 za fedha ni sawa na kilo 70.
Languages