Zaburi 87
Sifa Za Yerusalemu
Zaburi ya wana wa Kora. Wimbo.
1 Ameuweka msingi wake katika mlima mtakatifu;
2 Bwana anayapenda malango ya Sayuni
kuliko makao yote ya Yakobo.
3 Mambo matukufu yanasemwa juu yako,
ee mji wa Mungu:
4 “Nitaweka kumbukumbu ya Rahabu[a] na Babeli
miongoni mwa wale wanaonikubali mimi:
Ufilisti pia na Tiro, pamoja na Kushi,[b]
nami nitasema, ‘Huyu alizaliwa Sayuni.’ ”
5 Kuhusu Sayuni itasemwa hivi,
“Huyu na yule walizaliwa humo,
naye Aliye Juu Sana mwenyewe
atamwimarisha.”
6 Bwana ataandika katika orodha ya mataifa:
“Huyu alizaliwa Sayuni.”
7 Watakapokuwa wanapiga vinanda wataimba,
“Chemchemi zangu zote ziko kwako.”
<- Zaburi 86Zaburi 88 ->
Zaburi
a
-
Rahabu hapa ni jina la ushairi la Misri.
- b Kushi hapa ina maana ya Naili ya juu, yaani Ethiopia.