Link to home pageLanguagesLink to all Bible versions on this site
Zaburi 125
Usalama Wa Watu Wa Mungu
Wimbo wa kwenda juu.
1 Wale wamtumainio Bwana ni kama mlima Sayuni,
ambao hauwezi kutikisika, bali wadumu milele.
2 Kama milima inavyozunguka Yerusalemu,
ndivyo Bwana anavyowazunguka watu wake
sasa na hata milele.
 
3 Fimbo ya waovu haitadumu juu ya nchi
waliopewa wenye haki,
ili wenye haki wasije wakatumia
mikono yao kutenda ubaya.
 
4 Ee Bwana, watendee mema walio wema,
wale walio wanyofu wa moyo.
5 Bali wale wanaogeukia njia zilizopotoka,
Bwana atawafukuza pamoja na watenda mabaya.
 
Amani iwe juu ya Israeli.

<- Zaburi 124Zaburi 126 ->
  • Zaburi