Link to home pageLanguagesLink to all Bible versions on this site
2
Orodha Ya Watu Waliorudi Kutoka Uhamishoni
(Nehemia 7:4-73)
1 Basi hawa ndio watu wa jimbo waliotoka uhamishoni, ambao Nebukadneza mfalme wa Babeli alikuwa amewachukua mateka hadi Babeli (walirudi Yerusalemu na Yuda, kila mmoja kwenye mji wake, 2 wakiwa wamefuatana na Zerubabeli, Yeshua, Nehemia, Seraya, Reelaya, Mordekai, Bilshani, Mispari, Bigwai, Rehumu na Baana):
 
Orodha ya wanaume kati ya watu wa Israeli ilikuwa:
3 wazao wa Paroshi 2,172
4 wazao wa Shefatia 372
5 wazao wa Ara 775
6 wazao wa Pahath-Moabu (wa jamaa ya Yeshua na Yoabu) 2,812
7 wazao wa Elamu 1,254
8 wazao wa Zatu 945
9 wazao wa Zakai 760
10 wazao wa Bani 642
11 wazao wa Bebai 623
12 wazao wa Azgadi 1,222
13 wazao wa Adonikamu 666
14 wazao wa Bigwai 2,056
15 wazao wa Adini 454
16 wazao wa Ateri (kupitia Hezekia) 98
17 wazao wa Besai 323
18 wazao wa Yora 112
19 wazao wa Hashumu 223
20 wazao wa Gibari 95
 
41 Waimbaji:
wazao wa Asafu 128
 
42 Mabawabu wa lango la Hekalu:
wazao wa
Shalumu, Ateri, Talmoni,
Akubu, Hatita na Shobai
139
 
43 Watumishi wa Hekalu:[a]
wazao wa Siha, Hasufa, Tabaothi,
44 wazao wa Kerosi, Siaha, Padoni,
45 wazao wa Lebana, Hagaba, Akubu,
46 wazao wa Hagabu, Shalmai, Hanani,
47 wazao wa Gideli, Gahari, Reaya,
48 wazao wa Resini, Nekoda, Gazamu,
49 wazao wa Uza, Pasea, Besai,
50 wazao wa Asna, Meunimu, Nefusimu,
51 wazao wa Bakbuki, Hakufa, Harhuri,
52 wazao wa Basluthi, Mehida, Harsha,
53 wazao wa Barkosi, Sisera, Tema,
54 wazao wa Nesia na Hatifa.
 
55 Wazao wa watumishi wa Solomoni:
wazao wa Sotai, Hasaferethi, Peruda,
56 wazao wa Yaala, Darkoni, Gideli,
57 wazao wa Shefatia, Hatili, Pokereth-Hasebaimu na Ami.
 
58 Watumishi wa Hekalu wote na
wazao wa watumishi
wa Solomoni
392
 
59 Wafuatao walikuja kutoka miji ya Tel-Mela, Tel-Harsha, Kerubu, Adoni na Imeri, lakini hawakuweza kuthibitisha kwamba jamaa zao zilikuwa uzao wa Israeli:
60 wazao wa
Delaya, Tobia na Nekoda
652
 
61 Kutoka miongoni mwa makuhani:
Wazao wa Hobaya, Hakosi, Barzilai (mtu aliyekuwa amemwoa binti wa Barzilai, Mgileadi, naye akaitwa kwa jina hilo).
62 Hawa walitafuta orodha za jamaa zao, lakini hawakuonekana humo, kwa hiyo waliondolewa kutoka kundi la makuhani kwa kuwa walihesabiwa kuwa najisi. 63 Mtawala aliagiza kuwa wasile chochote miongoni mwa vyakula vitakatifu hadi kuwe kuhani atakayehudumu kwa Urimu na Thumimu.[b]
 
64 Jumla ya watu wote waliorudi walikuwa 42,360; 65 tena zaidi ya hao walikuwepo watumishi wa kiume na wa kike 7,337; pia walikuwamo waimbaji wanaume na wanawake 200. 66 Walikuwa na farasi 736, nyumbu 245, 67 ngamia 435 na punda 6,720.
 
68 Walipofika kwenye nyumba ya Bwana huko Yerusalemu, baadhi ya viongozi wa jamaa walitoa sadaka za hiari kwa ajili ya kujenga upya nyumba ya Mungu katika eneo lake. 69 Wakatoa kwa kadiri ya uwezo wao na kutia katika hazina darkoni 61,000[c] za dhahabu, mane 5,000[d] za fedha, na mavazi 100 ya ukuhani kwa ajili ya kazi hiyo.

70 Makuhani, Walawi, waimbaji, mabawabu, na watumishi wa Hekalu waliishi katika miji yao wenyewe, pamoja na baadhi ya watu wengine, nao Waisraeli waliosalia waliishi katika miji yao.

<- Ezra 1Ezra 3 ->
  • Ezra
  • <
  • 2
  • >

  • a Yaani Wanethini (pia 2:58, 70).

  • b Urimu na Thumimu maana yake ni Nuru na Kweli; vifaa hivi viliwekwa kwenye kifuko cha kifuani cha kisibau cha kuhani mkuu ili kujua mapenzi ya Mungu kwenye mambo ya kutatanisha.

  • c Darkoni 61,000 za dhahabu ni sawa na kilo 500.

  • d Mane 5,000 za fedha ni sawa na kilo 2,900.