7
Wana Wa Isakari
1 Wana wa Isakari walikuwa:
Tola, Pua, Yashubu na Shimroni; wote ni wanne.
2 Wana wa Tola walikuwa:
Uzi, Refaya, Yerieli, Yahmai, Ibsamu na Shemueli waliokuwa viongozi wa jamaa zao. Wakati wa utawala wa Mfalme Daudi, wazao wa Tola walioorodheshwa kama wapiganaji katika ukoo wao walikuwa watu 22,600.
3 Mwana wa Uzi alikuwa:
Izrahia.
Wana wa Izrahia walikuwa:
Mikaeli, Obadia, Yoeli na Ishia. Wote hawa watano walikuwa wakuu wao. 4 Kulingana na ukoo wa jamaa zao, walikuwa na watu hodari wa vita wapatao 36,000, kwa sababu walikuwa na wanawake na watoto wengi.
5 Jamaa ya watu waliokuwa wapiganaji hodari kutoka koo zote za Isakari, kama ilivyoorodheshwa katika ukoo wao, jumla yao walikuwa 87,000.
Wana Wa Benyamini
6 Wana watatu wa Benyamini walikuwa:
Bela, Bekeri na Yediaeli.
7 Wana wa Bela walikuwa:
Esboni, Uzi, Uzieli, Yeremothi na Iri; walikuwa viongozi wa jamaa zao; wote ni watano. Watu wapiganaji walioorodheshwa katika ukoo wao walikuwa 22,034.
8 Wana wa Bekeri walikuwa:
Zemira, Yoashi, Eliezeri, Elioenai, Omri, Yeremothi, Abiya, Anathothi na Alemethi. Hawa wote walikuwa wana wa Bekeri. 9 Orodha ya ukoo wao iliyoandikwa viongozi wa jamaa zao walikuwa wapiganaji 20,200.
10 Mwana wa Yediaeli alikuwa:
Bilhani.
Wana wa Bilhani walikuwa:
Yeushi, Benyamini, Ehudi, Kenaana, Zethani, Tarshishi na Ahishahari. 11 Hawa wana wote wa Yediaeli walikuwa viongozi wa jamaa zao. Kulikuwako wanaume wapiganaji 17,200 waliokuwa tayari kwenda vitani.
12 Washupimu na Wahupimu walikuwa wazao wa Iri. Wahushimu walikuwa wazao wa Aheri.
Wana Wa Naftali
13 Wana wa Naftali walikuwa:
Yahzieli, Guni, Yeseri na Shalumu; hao walikuwa wazao wa Bilha.
Wana Wa Manase
14 Wana wa Manase walikuwa:
Asirieli alikuwa mzao wake kutokana na suria wake wa Kiaramu. Huyu suria akamzaa Makiri baba wa Gileadi. 15 Makiri akatwaa mke kutoka miongoni mwa Wahupimu na Washupimu. Jina la dada yake aliitwa Maaka.
Mwana wa pili wa Makiri aliitwa Selofehadi, ambaye alikuwa na wasichana tu.
16 Maaka mkewe Makiri akamzaa mwana aliyemwita Pereshi. Jina la nduguye lilikuwa Shereshi. Wana wa Pereshi walikuwa Ulamu na Rakemu.
17 Mwana wa Ulamu alikuwa:
Bedani.
Hawa ndio waliokuwa wana wa Gileadi mwana wa Makiri, mwana wa Manase. 18 Dada yake aliyeitwa Hamolekethi aliwazaa Ish-Hodi, Abiezeri na Mahla.
19 Wana wa Shemida walikuwa:
Ahiani, Shekemu, Liki na Aniamu.
Wana Wa Efraimu
20 Wana wa Efraimu walikuwa:
Shuthela, ambaye alimzaa Beredi,
Beredi akamzaa Tahathi, Tahathi akazaa Eleada,
Eleada akamzaa Tahathi, 21 Tahathi akamzaa Zabadi,
na Zabadi akamzaa Shuthela.
Ezeri na Eleadi waliuawa na wenyeji wa Gathi walipokuwa wamekwenda huko kuwanyangʼanya mifugo yao. 22 Baba yao Efraimu akawaombolezea kwa siku nyingi, na jamaa zake wakaja kumfariji. 23 Kisha akakutana kimwili na mke wake tena, naye akachukua mimba, akamzalia mwana. Akamwita Beria, kwa sababu ya misiba iliyoipata nyumba yake. 24 Beria alikuwa na binti jina lake Sheera. Huyu ndiye aliijenga miji ya Beth-Horoni ya Juu na Beth-Horoni ya Chini, pamoja na Uzen-Sheera.
25 Beria akamzaa pia Refa, naye Refa akamzaa Reshefu,
Reshefu akamzaa Tela, Tela akamzaa Tahani,
26 Tahani akamzaa Ladani, Ladani akamzaa Amihudi,
Amihudi akamzaa Elishama, 27 Elishama akamzaa Nuni,
Nuni akamzaa Yoshua.
28 Nchi zao na makazi yao yalijumuisha Betheli na vijiji vilivyouzunguka, Naarani ilikuwa upande wa mashariki, Gezeri pamoja na vijiji vyake upande wa magharibi, pia Shekemu na vijiji vyake hadi kufikia Aya na vijiji vyake. 29 Katika mipaka ya Manase walikuwepo Beth-Shani, Taanaki, Megido na Dori pamoja na vijiji vyake. Wana wa Yosefu mwana wa Israeli waliishi katika miji hii.
Wana Wa Asheri
30 Wana wa Asheri walikuwa:
Imna, Ishva, Ishvi na Beria. Dada yao alikuwa Sera.
31 Wana wa Beria walikuwa:
Heberi na Malkieli, aliyekuwa baba yake Birzaithi.
32 Heberi akawazaa Yafleti, Shomeri na Hothamu, na Shua dada yao.
33 Wana wa Yafleti walikuwa:
Pasaki, Bimhali na Ashvathi.
Hawa walikuwa wana wa Yafleti.
34 Wana wa Shemeri walikuwa:
Ahi, Roga, Yehuba na Aramu.
35 Wana wa Helemu ndugu yake walikuwa:
Sofa, Imna, Sheleshi na Amali.
36 Wana wa Sofa walikuwa:
Sua, Harneferi, Shuali, Beri, Imra, 37 Bezeri, Hodu, Shama, Shilsha, Ithrani*Kwa jina lingine Yetheri. na Beera.
38 Wana wa Yetheri walikuwa:
Yefune, Pispa na Ara.
39 Wana wa Ula walikuwa:
Ara, Hanieli na Risia.1 Mambo Ya Nyakati
a
40 Hawa wote ndio waliokuwa wazao wa Asheri, viongozi wa jamaa zao, watu bora, mashujaa walio hodari na viongozi maarufu. Idadi ya watu waliokuwa tayari kwa vita, kama ilivyoorodheshwa katika ukoo wao, walikuwa 26,000.
<- 1 Mambo Ya Nyakati 61 Mambo Ya Nyakati 8 ->-
Kwa jina lingine Yetheri.