6
Wana Wa Lawi
1 Wana wa Lawi walikuwa:
Gershoni, Kohathi na Merari.
2 Wana wa Kohathi walikuwa:
Amramu, Ishari, Hebroni na Uzieli.
3 Amramu alikuwa na wana:
Aroni, Mose, na Miriamu.
Aroni alikuwa na wana:
Nadabu, Abihu, Eleazari na Ithamari.
4 Eleazari akamzaa Finehasi,
Finehasi akamzaa Abishua,
5 Abishua akamzaa Buki,
Buki akamzaa Uzi,
6 Uzi akamzaa Zerahia,
Zerahia akamzaa Merayothi,
7 Merayothi akamzaa Amaria,
Amaria akamzaa Ahitubu,
8 Ahitubu akamzaa Sadoki,
Sadoki akamzaa Ahimaasi,
9 Ahimaasi akamzaa Azaria,
Azaria akamzaa Yohanani,
10 Yohanani akamzaa Azaria (ndiye alifanya kazi ya ukuhani katika Hekalu alilojenga Mfalme Solomoni huko Yerusalemu),
11 Azaria akamzaa Amaria,
Amaria akamzaa Ahitubu,
12 Ahitubu akamzaa Sadoki,
Sadoki akamzaa Shalumu,
13 Shalumu akamzaa Hilkia,
Hilkia akamzaa Azaria,
14 Azaria akamzaa Seraya,
Seraya akamzaa Yehosadaki.
15 Yehosadaki alihamishwa wakati Bwana aliwapeleka uhamishoni watu wa Yuda na Yerusalemu kwa mkono wa Mfalme Nebukadneza.
16 Wana wa Lawi walikuwa:
Gershoni, Kohathi na Merari.
17 Haya ndiyo majina ya wana wa Gershoni:
Libni na Shimei.
18 Wana wa Kohathi walikuwa:
Amramu, Ishari, Hebroni na Uzieli.
19 Wana wa Merari walikuwa:
Mahli na Mushi.
Zifuatazo ni koo za Walawi zilizoorodheshwa kufuatana na baba zao:
20 Wazao wa Gershoni:
Gershoni akamzaa Libni, Libni akamzaa Yahathi,
Yahathi akamzaa Zima, 21 Zima akamzaa Yoa,
Yoa akamzaa Ido, Ido akamzaa Zera,
Zera akamzaa Yeatherai.
22 Wazao wa Kohathi:
Kohathi akamzaa Aminadabu, Aminadabu akamzaa Kora,
Kora akamzaa Asiri, 23 Asiri akamzaa Elikana,
Elikana akamzaa Ebiasafu, Ebiasafu akamzaa Asiri,
24 Asiri akamzaa Tahathi, Tahathi akamzaa Urieli,
Urieli akamzaa Uzia, Uzia akamzaa Shauli.
25 Wazao wa Elikana walikuwa:
Amasai na Ahimothi,
26 Ahimothi akamzaa Elikana, Elikana akamzaa Sofai,
Sofai akamzaa Nahathi, 27 Nahathi akamzaa Eliabu,
Eliabu akamzaa Yerohamu, Yerohamu akamzaa Elikana,
Elikana akamzaa Samweli.
28 Wana wa Samweli walikuwa:
Yoeli mzaliwa wake wa kwanza,
na Abiya mwanawe wa pili.
29 Wafuatao ndio wazao wa Merari:
Merari akamzaa Mahli, Mahli akamzaa Libni,
Libni akamzaa Shimei, Shimei akamzaa Uza,
30 Uza akamzaa Shimea, Shimea akamzaa Hagia,
Hagia akamzaa Asaya.
Waimbaji Wa Hekalu
31 Hawa ndio watu ambao Daudi aliwaweka kuwa viongozi wa uimbaji katika nyumba ya Bwana, baada ya Sanduku la Agano kuletwa ili kukaa huko. 32 Walihudumu kwa kuimba mbele ya Maskani, Hema la Kukutania, mpaka hapo Mfalme Solomoni alipojenga Hekalu la Bwana huko Yerusalemu. Walitimiza wajibu wao kulingana na taratibu walizokuwa wamewekewa.
33 Wafuatao ni watu waliohudumu pamoja na wana wao:
Kutoka ukoo wa Kohathi walikuwa:
Hemani, mpiga kinanda,
alikuwa mwana wa Yoeli, mwana wa Samweli,
34 mwana wa Elikana, mwana wa Yerohamu,
mwana wa Elieli, mwana wa Toa,
35 mwana wa Sufu, mwana wa Elikana,
mwana wa Mahathi, mwana wa Amasai,
36 mwana wa Elikana, mwana wa Yoeli,
mwana wa Azaria, mwana wa Sefania,
37 mwana wa Tahathi, mwana wa Asiri,
mwana wa Ebiasafu, mwana wa Kora,
38 mwana wa Ishari, mwana wa Kohathi,
mwana wa Lawi, mwana wa Israeli;
39 na msaidizi wa Hemani alikuwa Asafu, aliyesimama mkono wa kuume:
Asafu mwana wa Berekia, mwana wa Shimea,
40 mwana wa Mikaeli, mwana wa Baaseya,
mwana wa Malkiya, 41 mwana wa Ethni,
mwana wa Zera, mwana wa Adaya,
42 mwana wa Ethani, mwana wa Zima,
mwana wa Shimei, 43 mwana wa Yahathi,
mwana wa Gershoni, mwana wa Lawi.
44 Na kutoka kwa walioshirikiana nao, Wamerari, mkono wake wa kushoto:
Ethani mwana wa Kishi, mwana wa Abdi,
mwana wa Maluki, 45 mwana wa Hashabia,
mwana wa Amazia, mwana wa Hilkia,
46 mwana wa Amsi, mwana wa Bani,
mwana wa Shemeri, 47 mwana wa Mahli,
mwana wa Mushi, mwana wa Merari,
mwana wa Lawi.
48 Ndugu zao wengine Walawi walipewa huduma nyingine za kuhudumia hema takatifu, nyumba ya Mungu. 49 Lakini Aroni na uzao wake ndio waliokuwa na wajibu wa kutoa sadaka katika madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa na kwenye madhabahu ya kufukizia uvumba pamoja na yote yaliyofanyika pa Patakatifu, wakifanya upatanisho kwa ajili ya Israeli, sawasawa na yale yote aliyoagiza Mose mtumishi wa Mungu.
50 Hawa ndio waliokuwa wazao wa Aroni:
Aroni akamzaa Eleazari, Eleazari akamzaa Finehasi,
Finehasi akamzaa Abishua, 51 Abishua akamzaa Buki,
Buki akamzaa Uzi, Uzi akamzaa Zerahia,
52 Zerahia akamzaa Merayothi, Merayothi akamzaa Amaria,
Amaria akamzaa Ahitubu, 53 Ahitubu akamzaa Sadoki,
Sadoki akamzaa Ahimaasi.
54 Zifuatazo ni sehemu walizopewa ziwe nchi yao kwa ajili ya makazi yao (walipewa wazao wa Aroni waliotoka katika ukoo wa Wakohathi, kwa sababu kura ya kwanza iliwaangukia):
55 Walipewa Hebroni katika nchi ya Yuda pamoja na sehemu ya malisho inayouzunguka. 56 Lakini mashamba pamoja na vijiji vilivyouzunguka mji alipewa Kalebu mwana wa Yefune.
57 Kwa hiyo wazao wa Aroni walipewa miji ifuatayo pamoja na eneo la malisho: Hebroni (mji wa makimbilio), Libna, Yatiri, Eshtemoa, 58 Hileni, Debiri, 59 Ashani, Yuta na Beth-Shemeshi pamoja na maeneo yake ya malisho. 60 Kutoka kabila la Benyamini walipewa Gibeoni, Geba, Alemethi na Anathothi, pamoja na maeneo yake ya malisho.
Miji hii kumi na mitatu iligawanywa miongoni mwa koo za Wakohathi.
61 Wazao waliobaki wa Wakohathi walipewa miji kumi kutoka koo za nusu ya kabila la Manase.
62 Wazao wa Gershoni, ukoo kwa ukoo, walipewa miji kumi na mitatu kutoka kwa makabila ya Isakari, Asheri na Naftali kutoka sehemu ya kabila la Manase huko Bashani.
63 Wazao wa Merari, ukoo kwa ukoo walipewa miji kumi na miwili kutoka makabila ya Reubeni, Gadi na Zabuloni.
64 Kwa hiyo Waisraeli waliwapa Walawi miji hii pamoja na maeneo yake ya malisho. 65 Kutoka makabila ya Yuda, Simeoni na Benyamini walipewa miji iliyotajwa hapo juu.
66 Baadhi ya koo za Wakohathi walipewa kama nchi yao miji kutoka kabila la Efraimu.
67 Katika nchi ya vilima ya Efraimu walipewa Shekemu (mji wa makimbilio) na Gezeri, 68 Yokmeamu, Beth-Horoni, 69 Aiyaloni na Gath-Rimoni, pamoja na maeneo yake ya malisho.
70 Kutoka nusu ya kabila la Manase, Waisraeli waliwapa koo za Wakohathi waliobaki miji ya Aneri na Bileamu pamoja na maeneo yake ya malisho.
71 Wagershoni walipokea miji ifuatayo pamoja na maeneo yake ya malisho:
Katika nusu ya kabila la Manase:
walipewa Golani katika Bashani na pia Ashtarothi.
72 Kutoka kabila la Isakari
walipokea Kedeshi, Daberathi, 73 Ramothi na Anemu, pamoja na maeneo yake ya malisho.
74 Kutoka kabila la Asheri
walipokea Mashali, Abdoni, 75 Hukoki na Rehobu, pamoja na maeneo yake ya malisho.
76 Kutoka kabila la Naftali
walipokea Kedeshi katika Galilaya, Hamoni na Kiriathaimu pamoja na maeneo yake ya malisho.
77 Wamerari (Walawi waliobakia) walipokea miji ifuatayo:
kutoka kabila la Zabuloni
walipokea Yokneamu, Karta, Rimoni na Tabori pamoja na maeneo yake ya malisho.
78 Kutoka kabila la Reubeni, ngʼambo ya Yordani mashariki mwa Yeriko
walipokea Bezeri ulioko jangwani, Yahasa, 79 Kedemothi na Mefaathi pamoja na maeneo yake ya malisho.
80 Na kutoka kabila la Gadi
walipokea Ramothi huko Gileadi, Mahanaimu, 81 Heshboni na Yazeri, pamoja na maeneo yake ya malisho.
<- 1 Mambo Ya Nyakati 51 Mambo Ya Nyakati 7 ->
1 Mambo Ya Nyakati